Umoja wa mawakala wa mabasi stendi ndogo Kahama umesema kuwa watatoa gharama zote za kumchukulia fomu ya Urais mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Mapinduzi CCM Samia Suluhu Hassan.
Hayo yamesemwa kwenye risala yao mbele ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa wakati wa ufunguzi wa Shina la wakereketwa wa ccm la Mhe.Samia Suluhu Hassan la mawakala wa mabasi stendi ndogo-Majengo Kahama.
Mawakalawa hao wamesema kuwa wanafurahishwa na kazi anazozifanya Rais Samia Suluhu Hassan kwa watanzania ikiwemo uboreshaji wa barabara na ujenzi wa shule na vituo vya afya hali inayosaidia familia zao kupata huduma za elimu,afya pamoja na maji.
Wameongeza kuwa wao kama mawakala wa usafirishaji wanafurahi kuona barabara zinapitika pamoja na kurejeshwa kwa mikopo ya vijana,walemavu na kinamama na kwamba wao wanamuunga mkono kwa asilimi mia moja.
Akiongea na waandishi wa habari mlezi wa umoja huo Baraka Jilumbi amesema kuwa wameamua kufungua shina hilo kwa lengo la kumuunga mkono Rais Samia na kwamba wameamua kutoa gharama za kuchukua fomu ya urais 2025.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amewapongeza mawakala hao kwa hatua hiyo na kutoa wito wa kuimarisha umoja wao kwa manufaa ya kikundi chao.
Shina la wakereketwa wa ccm la Mhe.Samia Suluhu Hassan la mawakala wa mabasi stendi ndogo-Majengo Kahama lina wanachama zaidi y amia tatu (300) likijumuisha Mama lishe,wamachinga,wasafirishaji na wajasiliamali wengine
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akiwapongeza mawakala wa Mabasi Stendi ndogo Kahama.