TANZANIA imefanikiwa kukata tiketi
ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani
nchini Cameroon baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Sudan leo
Uwanja wa Omdurman, Mourada mjini Omdurman.
ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani
nchini Cameroon baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Sudan leo
Uwanja wa Omdurman, Mourada mjini Omdurman.
Shujaa wa Tanzania leo alikuwa ni mshambuliaji Ditram Nchimbi
aliyeongezwa kikosini baada ya mechi ya kwanza ambaye leo alisababisha
bao la kwanza na kufunga la pili.
Kwa matokeo hayo, Taifa Stars inayofundishwa na kocha Mrundi,
Etienne Ndayiragijje inafuzu CHAN ya 2020 kwa faida ya mabao ya ugenini
baada ya sare ya jumla ya 2-2, kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa
kwanza Dar es Salaam.
Hiyo inakuwa mara ya pili kwa
Taifa Stars kufuzu fainali za michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji
wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, baada ya mwaka 2009 nchini Ivory
Coast, ikiitoa Sudan pia katika raundi ya mwisho ya kufuzu.
Taifa Stars kufuzu fainali za michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji
wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, baada ya mwaka 2009 nchini Ivory
Coast, ikiitoa Sudan pia katika raundi ya mwisho ya kufuzu.
Sudan ilitangulia kwa bao la Amir Kamal dakika ya 30 akimalizia
krosi ya Ahmed Adam Mohamed aliyemlamba chenga beki wa kulia wa
Tanzania, Salum Kimenya.
Nchimbi akaangushwa nje kidogo ya boksi na mabeki wa Sudan
aliowazidi mbio na Nahodha, Erasto Edward Nyoni akaenda kufunga kwa
shuti la mpira wa adhabu dakika ya 49 kuisawazishia Taifa Stars.
Nchimbia aliyejumuishwa kikosini baada ya kufunga hat trick
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, timu yake Polisi ikitoa sare
ya 3-3 na vigogo, Yanga SC akafunga bao la ushindi dakika ya 79
akimalizia pasi ya mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda.
Furaha zaidi ni kwa kipa mkongwe wa Tanzania, Juma Kaseja
aliyerejeshwa kikosini baada ya miaka mitano, ambaye amedaka mechi zote
za kufuzu na kuipa tiketi ya CHAN nchi yake.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Juma Kaseja, Salum Kimenya,
Gardiel Michael, Erasto Nyoni, Bakari Kondo, Jonas Mkude, Miraj
Athumani/Ayoub Lyanga dk64, Frank Domayo/Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dk82,
Muzamil Yassin, Ditram Nchimbi na Iddi Suleiman ‘Nado’/Shaaban Iddi
Chilunda dk62.