Agizo la raisi latekelezwa kagera, ni kuhusu kuhama kwa halmashauri.

Na Silvia A Mchuruza.
Kufuati agizo la Rais wa awamu
ya tano  Dk.John Pombe Magufuri kuagiza halmashauri zote kuhama mjini na
kwenda maeneo ya vijijini,  alipokuwa katika ziara ya kikazi  mkoani
Rukwa katika wilaya ya sumbawanga mji mdogo wa Lahela ili kuhakikisha
wanatoa huduma kwa wananchi wanyonge.
Nae mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya ya bukoba vijijini Mh. Murshid Ngeze kwa kushirikia na madiwa wa
halmashauli hiyo wameafikiana kuhama haraka kutoka katika halmashauri
ya manispaa ya bukoba na kwenda katika eneo lililopangwa kwa ajili ya
halmashauli hiyo ikiwa ni kati ya halmashauri 31 ambazo azipo katika
maeneo ya kiutawa.
Hata hivyo halmashauri hiyo
iliweka watafiti hili kuhakikisha wanapata eneo linalofikikika kwa
urahisi kutoka kata zote za halmashauri ambapo walipendekeza maeneo
matatu ambayo ni eneo la kijiji Kanazi (BUJUNANGOMA),eneo la nyakatoke
kata Rubale pamoja naeneo la Kyema ambapo ni msitu wa halmashauri hiyo.
Aidha nao watafiti hao waliweza
kufanya kazi hiyo kwa kupima umbali wa kilimita na baadae kuwasilisha
katika baraza la madiwani  ambapo madiwani hao waliweza kupiga kura na
kulipendekeza eneo la kijiji Kanazi (BUJUNANGOMA) lililo na ukubwa wa
ekali 60 na kusema kuwa eneo hilo linafikika kwa urahisi ambapo lipo
karibu na mji wa Kemondo hivyo ni rahisi kwenye kufanya upangaji na
upanuzi wa mji.
Vilivile nae mbunge wa jimbo
hilo la Bukoba vijijini Jasson Rweikiza amepongeza juhudi za watafiti
waliofanya kazi ya utafiti na kuweza kipata eneo husika na linalofikika
kwa urahisi.
“Jambo hili la kuhama kwa
halmashauri sio jipya tumepewa siku 30 hata hivyo nakumbuka kipindi cha
nyuma aliwahi kuja Mh. waziri Mizengo Pinda aliwahi kusema ni kwanini
tupo mjini ikiwa sisi ni watumishi tunaopaswa kufanyia kazi vijijini
walipo wananchi tunaotakiwa kuwahudumia pia huko tunapo hamia kutakuwepo
fursa za kwekeza kwa wafanya biasharanaamini tutalitekelea agizo la
Rais wetu kwa sababu hata siku anatoa agizo hili nilikuepo pia”Alisema
Rweikiza.