Rais mhe. dkt. magufuli azindua safari za ndege za shirika la ndege la tanzania atcl za kutoka dar kwenda mpanda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono
wananchi wakati akiondoka kuelekea mkoani Dodoma kwa
kutumia usafiri wa shirika la ndege la ATCL mara baada ya
kumaliza ziara yake Mpanda mkoani Katavi.
Ndege ya ATCL aina ya Bombardier Q400
ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi huku
ikimwagiwa maji (water salute)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono
vikundi vya ngoma na kwaya vya Mpanda mkoani Katavi kabla ya
kuzindua safari za Shirika la ndege la Tanzania ATCL kutoka Dar
kwenda Mpanda mkoani Katavi leo tarehe 12/10/2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mke
wake Mama Janeth Magufuli, viongozi wa mkoa wa Katavi,
Wabunge, Mawaziri na viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM,
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa safari za Shirika la ndege la
Tanzania ATCL kutoka Dar kwenda Mpanda mkoani Katavi leo
tarehe 12/10/2019.