Wafanyakazi 10 wa obc watozwa faini ya milioni 100 kwa kosa la kufanyakazi nchini bila kuwa na vibali

Na Mwandishi Wetu, Arusha
HAKIMU Mkazi wa Mahakama  ya Wilaya Arusha Rose Ngoka
jana amewahukumu washitakiwa kumi ambao ni raia wa kigeni, kulipa
Sh.milioni 100  au kwenda jela miezi 12, kwa kosa kufanya kazi kampuni
ya uwindaji ya Oterlo Businness Coperation (OBC) bila kuwa na kibali cha
kufanya kazi nchini.

Raia
hao  wa kigeni ni  Darweshi Jumma, Riaz Aziz Khan, Mohammad Tayyab, Ali
Bakhash, Abdulrahman Mohammed, Martin Crasta, Imtiaz Feyaz, Arshad
Muhammad, Hamza Sharif na Zulfiqar Ali.

Image result for waarabu wa OBC

Related image
Mkurugenzi wa OBC Issack Mollel akifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kutokana na mashtaka ya uhujumu uchumi yanayomkabili pamoja na kuajiri raia wa kigeni bila ya kuwa na vibali

Hakimu
Ngoka alisema mahakama imewatia hatiani washitakiwa hao kwa kukiri
kufanya kosa hilo nchini na kuamuru kila mmoja kulipa faini ya
Sh.milioni 10 au kwenda jela miezi 12.

“Lakini
kwa kuzingatia maombi ya Wakili wenu wa utetezi Steven Mosha na kwa
kuangalia  mazingira ya kesi na madhara ya kijamii kama alivyosema
mahakama imekata hatiani na kuwapa adabu hiyo ili iwe fundisho kwa
wengine,”alisema

Ngoka
mbali na kuwapa adhabu ya kulipa faini,pia aliwaonya washitakiwa hao na
kuwataka kutii sheria,kanuni na taratibu za nchi pindi wanapoingia
nchini.

Wakili wa utetezi
Steven Mosha kabla ya hukumu hiyo kutolewa aliomba Mahakama hiyo kuwapa
adhabu ndogo washitakiwa hao kwa sababu ni kosa lao la kwanza kufanya.

“Lakini
naomba iwapunguzie adhabu sababu wamekiri na kuokoa muda wa
mahakama,lakini pia washitakiwa wawili wana utaifa wa nchi ya India na
nane raia wa Pakstani na walishitakiwa miezi mingi nyuma na kutumia
gharama kubwa za kuishi,”alisema

Alisema
kutokana na kushitakiwa wamelazimika kutumia fedha nyingi katika kuishi
nchini na wengi wao vijana wanahitajika katika taifa lao kujenga taifa.

“Lakini Hakimu naomba wape adhabu ndogo sababu wengine umri wao mkubwa wanahitaji  kukaa wanafamiliya zao,”alisema

Aidha
alisema kuwapa adhabu kubwa itasababisha ugumu wa maisha kwa familiya
zao,hivyo aliomba wapewa adhabu ya kulipa fedha kwa sababu wapo tayari
kulipa kiasi chochote cha fedha ambacho mahakama hiyo itaamuru.

Kabla
ya Wakili wa utetezi kutoa  maombi hayo Wakili Mkuu wa Serikali
Maritenus Marandu alisema  kabla ya jana washitakiwa hao waliandika
barua iliyowasilishwa na Wakili wao Steven Mosha  ikionyesha washitakiwa
hao kukiri makosa yao.

Pia
aliiambia  mahakamani hiyo kuwa, upande wa Jamuhuri hauna kumbukumbu za
makosa ya nyuma,ila aliomba mahakama iwape adhabu inayostahili
kulingana na kosa walilofanya.

Akiwakumbusha
washitakiwa hao makosa yao Wakili Mwandamizi wa serikali Mkoa wa Arusha
Abdallah Chavula akiwa na Wakili Idara ya Kazi Arusha Emmanuel Mweta
alisema washitakiwa hao walifanya kosa la kufanya kazi nchini bila
vibali vya kazi kati ya  Novemba 2018  na  Januari 2019.

Alisema washitakiwa hao wenye taaluma mbalimbali walikamatwa wakiwa na hatia zao zà kusafiria  wakijiandaa kuondoka nchini.

Washitakiwa
hao walikamatwa  Januari mwaka huu na Septemba 2 mwaka huu kesi hiyo 
ilifutwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi  Mfawidhi  Arusha
Niku Mwakatobe kutokana na Wakili wa  serikali kutokuwa tayari kuwasomea
hoja za awali ili kesi iendelee.

Wakati
huo huo mshitakiwa wa kwanza  Isaya  Mollel katika kesi hiyo ambaye ni
Mkurugenzi wa OBC anayekabiliwa  na kosa la kuajiri raia hao wa  kigeni,
bila ya kuwa na vibali kwa mujibu wa sheria za nchi za kutoa ajira kwa
wageni hajakiri kosa na amepangiwa kesi yake Oktoba 16  mwaka huu.

Washitakiwa hao walifanikiwa kulipa faini hiyo na kuachwa huru.

 Image result for waarabu wa OBC