Kabudi: tanzania tumedhamiria kubadili maisha ya watu wetu

Waziri
wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Profesa
Palamagamba John Kabudi amesema Tanzania imedhamiria kubadili maisha ya
wananchi wake ikijitahidi kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDGs.


Akihutubia
mjadala Mkuu wa Baraza Kuu laUmoja wa Mataifa kikao cha 74 mjini New
York Marekani Ijumaa usiku Profesa Kabudi amesema Tanzania imeweka
ajenda kuu za kuzitekeleza ambazo ni pamoja na “kutokomeza ufisadi,
kurejesha haki na heshma katika sekta za umma, na kuimarisha ukusanyaji
kodi kama mbinu ya kufikiwa kwa haraka ukuaji wa kiuchumi.” 


Mengine wanayoyapa kipaumbele ni “elimu bora kwa wote, huduma za afya, na uwajibikaji.”
Waziri huyo amesema  hivi juhudi hizo pia zinalenga kuboresha kiwango
cha elimu nchini , kutokomeza umasikini, na kukabiliana na kushughulikia
tatizo la ajira, uandikishaji watoto wanaoingia shule kimepanda kwa
asilimia 35.2 ikiwa imechangiwa na hatua ya serikali ya kutoa elimu bure
kwa shule za msingi hadi kitato cha nne.
Hatua zinazochukuliwa
Waziri Kabudi amesema serikali imechukua hatua madhubuti kukabiliana na
ufisadi ambazo ni pamoja na “kuanzisha kitengo cha kupambana na uhalifu
na ufisadi katika mahakama kuu, na kuimarisha suala la uwajibikaji na
uwazi katika serikali. “
Katika miaka minne iliyopita Profesa Kabudi amesema serikali imetekeleza
mabadiliko kadhaa yanayojumuisha kudhibiti utajiri na mali asili ya
nchi hiyo kwa kupitia mikataba mbalimbali na hatua hizo zitasaidia
kuongeza pato la taifa kwa ukusanyaji mapato, pia sheria mpya za madini
zimeisaidia Tanzania kukusanya mabilioni ya fedha ambayo yameisaidia
serikali kuongeza kiasi cha bajeti yake hadi asilimia 40 mwaka 2019
ukilinganisha na asilia 25 mwaka 2016.
Profesa Kabudi ameongeza kuwa mapato hayo yamesaidia kuboresha miradi
mbalimbali ya miundombinu na kuinua hali ya wananchi kuanzia katika
afya, maji, na usafi. Hatua hizo pia zimesaida kutoa elimu bure kwa
shule za umma za msingi na sekondari akitolea mfani shule za msingi
uandikishaji Watoto umeongezeka kwa asilimia 35.2.
Amesema serikali pia inahakikisha uhifadhi mazingira na kujumuisha kila
mwananchi katika mchakato wa SDGs ikiwemo makundi yasiyojiweza.
Na katika upande wa nishati ambayo awali ilikuwa ni bidhaa adimu sasa
takriban asilimia 67 ya wananchi wa Tanzania wana nishati ya umeme
kutokana na mradi maalum wa kusambaza umeme vijijini, REA .
Pia kuna ujenzi wa bwawa kubwa kabisa la kuzalisha umeme unaoendelea 
ambao utakuwa  mkombozi sio tu kwa wananchi wa taifa hilo bali hata nchi
jirani.
Pia amesema mbali ya uhifadhi wa mazingira kuna masuala mengine
yanayozingatiwa ikiwemo nishati endelevu na kuhakikisha teknolojia hiyo
inawasaidia mengi.
Uhuru wa vyombo vya habari
Prosesa Kabudi amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika suala la
uhuru wa vyombo vya habari na kuongeza kiwango cha utoaji leseni
akitolea mfano kwamba taifa hilo lina jumla ya vituo vya redio 152 na ni
vitatu tu ndivyo vinamilikiwa na serikali, huku vituo vya televisheni
vikiwa 34 na viwili tu ndivyo vinavyomilikiwa na serikali. Kwa upande wa
magazeti serikali imetoa jumla ya leseni 172.
Na mwisho ametoa wito kwa nchi zote wanachama kukumbatia ushirikiano wa
kimataifa sio tu kwa ajili ya kutomoza umasikini, kuboresha kiwango cha
elimu, kukabiliana na mabadiliko yatabianchi na kufikia uwajibikaji bali
pia katika kudumisha amani na usalama lakini pia katika kuleta haki na
kuwa na dunia bora.