Serikali yafanya mkutano wa ushawishi na utetezi wa masuala ya watu wenye ulemavu katika ngazi ya wizara

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Watu Wenye
Ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.Philibert Kawemama akifungua mkutano kuhusu
ushawishi na utetezi wa masuala ya watu wenye ulemavu katika ngazi ya wizara
uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora jijini
Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Utawala, Ofisi ya Rais,
Utumishi na Utawala Bora Bi. Mwanaheri Cheyo.
Washiriki wa mkutano kuhusu ushawishi na utetezi wa
masuala ya watu wenye ulemavu katika ngazi ya wizara wakifuatilia mada katika
ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye
Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Bi.Ummy Nderiananga (kushoto) akiwasilisha  mada wakati wa mkutano kuhusu ushawishi na
utetezi wa masuala ya watu wenye ulemavu katika ngazi ya wizara uliofanyika
katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Agnes Meena
(kushoto) akichangia  mada wakati wa
mkutano kuhusu ushawishi na utetezi wa masuala ya watu wenye ulemavu katika
ngazi ya wizara uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala
Bora jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika akitoa
ufafanuzi kuhusu ushawishi na utetezi wa masuala ya watu wenye ulemavu katika
ngazi ya wizara kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na
Utawala Bora jijini Dodoma.