Mwigulu aanza ziara jimboni iramba, awataka wananchi kuunga mkono juhudi za rais magufuli

Mbunge
wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi jimboni
humo wakati akiwa ameanza ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za
maendeleo na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi. (Picha Zote Na
Innocent Natai, WazoHuru Blog)
Mbunge
wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba akishirikiana na wananchi kushusha
vifaa alivyoahidi jimboni humo wakati akiwa ameanza ziara ya kikazi ya
kukagua shughuli za maendeleo na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha
Mapinduzi.
Gari iliyobeba vifaa mbalimbali ikiwemo misumari, rangi, jipsam, na mabati ikishusha vifaa hivyo kwa ajili ya kutimiza ahadi ya Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba aliyoitoa hivi karibuni.
Mbunge
wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi jimboni
humo wakati akiwa ameanza ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za
maendeleo na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Na Innocent Natai, WazoHuru Blog-Iramba

Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba ametimiza ahadi zake alizo zitoa jimboni kwake Iramba Magharibi Aprili mwaka huu, ameyasema hayo hivi leo alipokuwa akikabidhi shehena ya vifaa kwaajili ya umaliziaji wa jengo la zahanati na shule yaliyo ezuliwa na upepo Aprili 2019.
Mwigulu amesema kuwa ameyafanya hayo baada ya ahadi

yake na maombi aliyoyapata kutoka kwa wananchi alipofanya ziara Aprili mwaka huu kwenye maeneo hayo kushuhudia madhara ya upepo ulioezua paa la hosipitali.


Baadhi ya vifaa alivyotoa mbunge huyo kwaajili ya zahanati Doromonyi ni pamoja na mbao kwaajili ya kuwekea paa, misumari, rangi, jipsam,mabati na chuma.
Mwigulu amesema kuwa pia aliamua kutoa saruji shule ya msingi Mikilango mifuko hamsini kwaajili ya kusaidia kuweka sakafu katika madarasa matatu yaliyokuwa yameharibika.
Mwigulu amewataka wananchi kuacha kuutolea maneno

mabaya mradi wa usambazaji umeme vijijini ujulikanao kama REA kwa kusema kuwa wanaweka nguzo na kuziacha bila kuweka nyaya bali amewataka kuwa na subira wakati watendaji wakuu wa mradi huo wakiendelea na usambazaji wa nguzo na nyaya kwa awamu kufuatana na jinsi utaalamu wa uwekaji ulivyo.


Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dokta John Pombe Magufuli imefanya kazi  kubwa kuhakikisha vijiji zaidi ya elfu saba vinapata umeme ukilinganisha na ilivyokuwa awali.
“Tumuunge mkono Rais wetu huwa halali anakesha kuhakikisha wananchi wake mnapata maendeleo kwasasa kwa maendeleo yoote aliyoyafanya yameshazidi asilimia ya ilani iliyowekwa kwenye ilani ya CCM’’ alisema Nchemba.
Kuhusu miundombinu ya barabara amezidi kumshukuru

Rais kwa kuwezeshwa kujengwa kwa barabara katika jimbo lake na kuzipandisha viwango barabara ambazo zilikuwa na hali mbaya na kushindwa kupitika kipindi cha mvua.

Mwigulu anatarajiwa kufanya ziara yake kwa siku kadhaa kwenye jimbo lake akikagua miradi mbalimbali ikiwemo ya

Shule,Barabara,Hospitali na mingine ya kijamii na pia kusikiliza kero mbalimbali za wapigakura wa jimbo la Iramba Mgharibi na kuzifanyia utautuzi.