Mambo 10 wanayozungumza wachambuzi wa soka mechi ya yanga vs zesco jana

Image result for yanga vs zesco
1: Zesco walikua bora sana kimbinu. Walienjoy mchezo Ugenini pengine kuliko watakavyoenjoy watakavyokua kwao. Respect LwandaminaπŸ™Œ

2: Zahera alikuja na mbinu ya ugenini katika uwanja wa nyumbani. Timu ilikua machachari katikati ya uwanjani lakini ilikua poor kwenye umaliziaji. Yanga ina shida ya mbinu.

3: Sadney ni yuleyule. Anakuwepo kwenye nafasi, lakini anachofanya kwenye hiyo nafasi baada ya kupokea mpira ni kichekesho. Sielewi kwanini bado yuko ‘First Eleven’ mpaka leo.

4: Thaban Kamusoko πŸ™Œ Cool. Calm. Collected. Alikua bora sana katikati ya uwanja kutuliza tempo ya viungo machachari wa Yanga.

5: Makame AbdulAziz… Alikua bora kwenye kupokonya mipira, kupiga pasi ndefu, lakini alikosa utulivu. Presha ya game ilimuingia. Kama Zesco wangekua makini, makosa ya Makame yalikua zawadi kwao.


Image result for yanga vs zesco

6: Lamine Moro.. What a ManπŸ™Œ Beki Kiongozi. Anajitoa. Alifanya kazi kubwa sana kuziba makosa ya Sonso na Balama kwenye kukaba.

7: Balama Mapinduzi πŸ€” Kama akiendelea kukaa na Zahera kwa wiki 10 zijazo, Tanzania itapoteza mmoja kati ya viungo bora sana wa ushambuliaji. Katika mbinu yoyote, Balama hawezi kua beki namba 2. Tusidanganyane.

8: Kwenye ripoti ya Zahera,  Ally Ally alisajiliwa kama beki namba 2. Swali la kwanza la Msolla kwa Zahera linabidi lianzie hapa.. Mwinyi alitumia kiungo gani cha mwili kumtazama Ally Ally kama beki wa pembeni? .
.
9: SibomanaπŸ€” Ni mfano mwingine wa wachezaji bora walioporomoka viwango kwa kasi. Nini shida? Kwangu ni mbinu. Nowdays, anatumika zaidi kwenye kulinda na kunyimwa uhuru wake wa kushambulia.

10: Metacha MnataπŸ€” Alicheza mechi ya CAF akiwa na akili ya VPL.. Unapotezaje muda kipindi cha kwanza tena ukiwa nyumbani? .
.
Nb: Bila shaka Kalengo waliyemtaka Yanga ni yule aliyevaa jezi ya Zesco.. Sio huyu aliyekujaπŸ˜€

Point namba 10 imenifanya nicheke🀣🀣🀣🀣🀣