Tbl yaadhimisha siku ya unywaji bia duniani kistaarabu, yakutanisha wafanyakazi wake

Wafanyakazi wa Comfort hotel Mbeya wakifuatilia mafunzo
Wafanyakazi wa TBL Arusha wakionyesha mabango ya uhamasishaji.
Wafanyakazi wa baa ya Kwetu Pazuri wakifuatilia mafunzo.
Wafanyakazi wa TBL Mwanza wakionyesha mabango ya uhamasishaji wakati wa maadhimisho hayo.
Afisa Masoko wa TBL kiwanda cha
Mwanza , Happy Conrad, akitoa elimu ya kunywa kistaarabu kwa wahudumu wa
baa ya Las Vegas, iliyopo Bwiru jijini Mwanza.

Meneja Masuala Endelevu wa TBL,Irene Mutiganzi,akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa baa ya Tips iliyopo Mikocheni Dar es Salaam.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imefanya maadhimisho ya Siku ya Bia Duniani 2019,
(Global Beer Responsible Day), ambapo wafanyakazi wake kutoka viwanda
vya Dar Es Salaam,Mwanza, Mbeya na Arusha, wameshiriki kufanya
uhamasishaji wa unywaji wa bia kistaarabu kwa wateja na wafanyakazi
katika mabaa mbalimbali.

Kauli mbiu ya  maadhimisho hayo ambayo wateja wake wengi wameyafurahia ni  100% Jiachie .100% Kwa kiasi. # Jipimie!)