Ttb yasaka soko la utalii korea kusini.

 Mkurugenzi  Mtendaji wa Bodi ya
Utalii Tanzania(TTB), Bi.Devota Mdachi akifafanua jambo kwa Waandishi wa
Habari (hawapo pichani)  Kuhusu ujio wa Waandishi wa Habari wa Haedan Media na Kituo cha Televishioni cha KBS
kutoka nchini Korea Kusini, Bw.Changmin Shin (kulia) na Bw.Sanghoon Ryu
(Kushoto) waliotembelea nchini kuangalia maeneo ya utalii.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania(TTB), Bi.Devota Mdachi akimpatia zawadi Mwandishi Sanghoon Ryu kutoka Haedan Media na Kituo cha Televishioni cha KBS mara baada ya Mkutano na Waandishi wa Habari  leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania(TTB), Bi.Devota Mdachi akimpatia zawadi Mwandishi Changmin Shin kutoka Haedan Media na Kituo cha Televishioni cha KBS mara baada ya Mkutano na Waandishi wa Habari  leo Jijini Dar es Salaam.
……………..
Na.Mwandishi Watu-MAELEZO
Serikali kupitia Bodi ya
Utalii Tanzania (TTB) imeendelea kuimarisha Sekta ya utalii nchini kwa
kutafuta masoko kwa wingi nchini za Mashariki ya mbali ili kuongeza wigo
wa soko la utalii katika nchini hizo.

 Akizungumza na Waandishi wa
Habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Devota Mdachi
alisema kuwa juhudi za kutafuta soko kwa nchi hizo zilizoko mashariki ya
mabli ni zitaimarisha  kuwepo kwa safari za Shirika la Ndege
Tanzania(ATCL) ambazo zitaanza kuleta watalii kutoka nchi hizo.

“Soko la Utalii la Korea
Kusini ni moja ya masoko yanayokuwa kwa kasi na sisi kama TTB tumepanga
mikakati madhubuti itakayo ongeza idadi ya watalii kutoka huu wa Korea
Kusini kwani takwimu zinaeleza wazi kuwa mwaka 2018 watalii kutoka nchi
hiyo waliongezeka kufikia 8,083 ikilinganishwa  na watalii 7,640 mwaka
2017” Alisema Mdachi.

Mdachi alisema kuwa TTB
inampango Mkakati wa kuwezesha kuongeza watalii kutoka korea ya kusini
ikiwemo kutumia mtandao Naver  wenye wafuasi wengi zaidi nchini humo,
asilimia 75 ya wananchi wa Korea Kusini hutumia mtandao huo kuangalia
taarifa mbalimbali zikiwemo zile za utalii.

Mikakati mingine ni kuandaa
ziara za mawakala wa utalii, kualika baadhi ya Vyombo vya Habari vya
Korea Kusini vyenye watazamaji wengi na kushiriki katika onesho la
utalii la Korea Kusini (KOTFA) pamoja na kuandaa safari za utangazaji
utalii katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Korea ya Kusini.

“Utekeleza wa Mikakati hiyo
tayari ulishaanza ambapo TTB kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania
Nchini Korea ya Kusini, tumeanzisha kampeni Maalum ya Kutangaza utalii
katika nchi hiyo na tumeanza kufanikiwa baada ya kupata ugeni wa
Waandishi wa Habari kutoka kampuni ya Haedan Media  na Kituo cha Televisheni cha KBS kutoka Korea Kusini ambao walikuwepo nchini kwa ziara ya siku 10”, Alisema Mdachi.

Watalaam hao walitembelea
maeneo mbalimbali ikiwemo Jiji la Arusha ambapo walitembelea  Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti, Ziwa Natroni, Ziwa Manyara na baada ya hapo
walienda Zanzibar na sasa wapo katika Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya
kutembelea Jiji hilo.