Breaking news: maxence mello wa jamii forum aibuka mshindi tuzo ya mwangosi 2019

Mkurugenzi Mkuu wa Jamii Forums Maxence
Mello (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 baada ya
Jamii Forums kuibuka mshindi wa Tuzo ya Daudi Mwangosi 2019 kutoka kwa
Balozi wa Sweden nchni,Anders Sjoberg katika ukumbi wa Rahaleo, Zanzibar,wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan


 KUTOKA ZANZIBAR
Mkurugenzi Mkuu wa Jamii Forums Maxence
Mello, ameibuka mshindiwa tuzo ya Mwangosi mwaka 2019, kutokana na umahiri aliouonyesha katika tasnia ya habari kwa kipindi cha mwaka jana.



Tuzo
hiyo hutolewa kila mwaka na Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari
Tanzania(UTPC) kumkumbuka Daudi Mwangosi aliyeuawa akiwa kazini Septemba
2, 2012 kijijini Nyololo mkoa wa Iringa akitekeleza majukumu yake ya
kikazi

Mwangosi ambaye alikuwa Mwenyekiti  wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa aliuwawa na Askari wa jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia baada ya kudaiwa kurushiwa bomu.





Balozi wa Sweden nchini Tanzania,Anders Sjoberg akimkabidhi tuzo ya
Daudi Mwangosi,Mkurugenzi  Mtendaji wa Jamii Media inayomiliki Mtandao
wa Jamii Forums, Maxence Mello leo katika ukumbi wa Raha Leo,Zanzibar .

Mkurugenzi  Mtendaji wa Jamii Media inayomiliki Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Mello akiangalia tuzo.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Jamii Media inayomiliki Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Mello akionesha  tuzo ya Daudi Mwangosi 2019.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Jamii Media inayomiliki Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Mello akionesha  tuzo ya Daudi Mwangosi 2019.

Balozi wa Sweden nchini Tanzania,Anders Sjoberg akimkabidhi hundi ya
shilingi milioni 10 Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media inayomiliki
Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Mello kwa kushinda tuzo ya Daudi
Mwangosi 2019.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Jamii Media inayomiliki Mtandao wa Jamii Forums,
Maxence Mello akipokea hundi ya shilingi milioni 10 ambayo ni zawadi ya
Tuzo ya Daudi Mwangosi 2019.