Wataalam wa mionzi wakutana jijini arusha, wajadili usalama wa kuhifadhi mabaki ya vyanzo vya mionzi

Mikidadi Swalehe ni
mkuu wa kitengo cha uhifadhi wa mabaki ya vyanzo vya mionzi ,katika
Tume ya nguvu za Atomic (TAEC)Nchini ambaye pia ni mratibu wa mkutano
huo unaoendelea Jijini Arusha,akizungumza na waandishi wa habari.Picha
na Vero Ignatus.
Mkutano
wa majadiliano ya namna ya kutatua changamoto na namna ya kuhifadhi  na
kuboresha usalama wa mabaki ya vyanzo vya mabaki ya mionzi unaofanyika
Jijini Arusha.
Washiriki
mbalimbali wa mkutano wa siku,tano wa majadiliano kama wanavyoonekana
katika picha pamoja na uwakikishi wa mataifa waliyotoka.
Mwakilishi wa Shirika la Nguvu za Atomiki,Duniani,David  Bannet  David  Bannet  akitoa salamu ya shirika hilo ambalo ni mwangalizi wa Kimataifa wa masuala ya matumizi ya teknolojia ya Nyuklia
Baadhi
ya washiriki kutoka nchi mbalimbali kama inavyoonekana katika meza zao
waliohudhuria mkutano wa siku tano unaoendelea Jijini Arusha katika
hotel ya Corido Spring Jijini Arusha.
Mkutano wa majadiliano ukiendelea katika Hoteli ya Corido Spring Jijini Arusha ambapo TAEC ndiyo mwenyeji wa mkutano huo.
Mkutano
wa majadiliano ya namna ya kutatua changamoto na namna ya kuhifadhi  na
kuboresha usalama wa mabaki ya vyanzo vya mabaki ya mionzi unaofanyika
Jijini Arusha.
Na.Vero Ignatus,Arusha.

Mkutano
wa Kimataifa kwaajili ya kujadili mikakati mbalimbali ya kuboresha
usalama katika kuhifadhi mabaki ya vyanzo vya mionzi ,unaendelea Jijini
Arusha na kukutanisha wataalam wa teknolojia ya nyuklia ,katika kujadili
changamoto za usalama wakati wa uhifadhi wa mabaki hayo,ili kuepusha
madhara kwa binadamu  na mazingira

Mikidadi Swalehe ni
mkuu wa kitengo cha uhifadhi wa mabaki ya vyanzo vya mionzi ,katika
Tume ya nguvu za Atomic (TAEC)Nchini,amesema kuwa mkutano huo
umehudhuriwa na wanachama 30 ,kutoka nchi 21 duniani,ambapo umelenga
katika kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti vyanzo vilivyomaliza muda
wake lakini bado vinatoa mionzi.

 Mikidadi amesema
jukumu la kusimamia usalama linahitaji nchi zote duniani ,kuhakikisha
kwamba, vyanzo vyote vya mionzi vinakuwa katika mikono salama,ili
kuepuka madhara mbalimbali ikiwemo kutumika kwa vyanzo hivyo katika
masuala ya ugaidi.

Amesema
kuwa vyanzo vya mionzi vilivyomaliza matumizi vinahitajika kuhifadhiwa
mahali salama  palipo na ulinzi maalum,kwani hali hiyo itasaidia
kuepusha vyanzo hivyo kuzagaa na kusababisha madhara mbalimbali kwa
binadamu,na mazingira ,amesema TAEC inalo jengo maalumu kwaajili ya
kuhifadhia vifaa hivyo vilivyomaliza matumizi yake.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA)  David  Bannet  akitoa
salamu ya shirika hilo ambalo ni mwangalizi wa Kimataifa wa masuala ya
matumizi ya teknolojia ya Nyuklia ,aliishukur Tanzania hususani TAEC
kukubali kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

Aidha
amesisitiza kuwa  IAEA  itaendelea kushirikiana na nchi wanachama
kuhakikisha kuwa teknolojia ya nyuklia itatumika kwa matumizi  salama
ili isiathiri binadamu wa vizazi vilivyopo sasa na vijavyo.

Awali mkutano huo wa siku tano ulifunguliwa na Mkurugenzi mkuu wa TAEC Nhini Profesa Lazaro Busagala ambapo unatarajiwa kumalizika kesho