Dkt. chaula aipongeza timu ya watoa huduma za dharura sadc

Katibu Mkuu Dkt.Zainabu Chaula akiwa kwenye picha ya pamoja na wayoa huduma za dharura waloshiriki mkutano wa 39 wa SADC
…………….
Na.Catherine Sungura,WAMJW
Katibu Mkuu,Wizara ya Afya Dkt.Zainabu Chaula amewapongeza timu ya wizara ya afya , taasisi zake pamoja na manispaa ambao walishiriki kutoa huduma kwenye mkutano wa 39 wa SADC ulomalizika leo jijini Dar es Salaam.
Dkt.Chaula ametoa pongezi hizo baada ya kumalizika kwa mkutano huo na kukutana na timu  hiyo na kufanya mazungumzo na watumishi hao.
“Mmefanya kazi kubwa na nzuri sana katika utoaji huduma kwenye mkutano huu hakika mnastahili pongezi”.Alisema Dkt.Chaula.
Aidha, Katibu Mkuu huyo alisema kama mtendaji mkuu atatafuta namna ya kuwawezesha watoa huduma wengine kujengewa uwezo na timu hiyo mahali walipotoka  ili kutembea pamoja katika kutekeleza mikakati ya sekta ya afya katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania kwani wamepata  ujuzi wa kutoa huduma hususani za dharura .
Timu hiyo ya kutoa huduma za dharura iliwajumlisha wataalam mbalimbali kutoka wizara ya afya,hospitali ya Taifa Muhimbili,Taasisi ya Mifupa(MOI), Taasisi ya Moyo(JKCI) pamoja na wataalam wengine kutoka hospitali za Manispaa  za Ubungo,Ilala,Kigamboni,Kinondoni na Temeke