Mbunge wa viti maalum amina mollel atoa msaada wa vifaa vya ujenzi kusaidia miundo mbinu ya shule

Na Mwandishi Wetu, APC BLOG, ARUSHA 
 
Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mollel Mkoani Arusha jana ametoa vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya sementi 150 pamoja na bati 48 ili kusaidia ujenzi wa miundombinu ya shule katika halmashauri ya Arusha DC vyenye thamani ya shilingi milioni tatu na nusu (3,500,000).
Mbunge huyo ametoa mifuko 30 pamoja na bati 38 katika shule ya sekondari ya olemedeye ili visaidie kukamilisha ujenzi kwenye madarasa mawili yanayotarajiwa kutumiwa na wanafunzi wa kitado cha kwanza mapema mwaka ujao wa 2020 huku katika shule ya Msingi ya Oldenderet wakipat mifuko 20 ya sementi. 
Aidha akiwa katika ziara yake katika kata ya Oldonyowas Mkoani humo, Mbunge Amina amechangia mifuko 20 ya sementi katika shule ya Msingi Losinoni ili isaidie ujenzi wa choo cha waalimu shuleni hapo.
Hata hivyo katika kutambua hali ya watoto wa kike katika kipindi Chao cha hedhi wengi wao kukosa masomo katika shule mbalimbali nchini, Mbunge huyo ametoa  mifuko 25 ya sementi katika shule ya Msingi Mringa kwa ajili ya  ujenzi wa vyumba  viwili vya kujihifadhi watoto wa kike wanapokuwa kwenye  hedhi.

Add caption