Wajumbe sadc wasifu juhudi za serikali kuhamasisha uwekezaji wa viwanda


Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies , Sailesh Pandit akisoma hotuba yake fupi mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies Sailesh Pandit ,akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari walioambatana na Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 

Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit  (pili kushoto) akionesha kipande cha nondo huku akieleza namna ambavyo hutengenezwa hatua kwa hatua na hatimaye kupelekwa sokoni kwa kuuzwa,mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  waliotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
  Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  wakiangalia namna nondo zinavyotengenezwa hatua kwa hatua ndani ya kiwanda cha Lodhia Group of Companies kilichopo MKuranga mkoani Pwani.Wajumbe hao wametembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit (kulia) akiwa na Meneja wa kiwanda hicho Harminder Bhachu wakiwaongoza Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC waliofika kutembelea kiwanda hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit  akieleza kuhusu namna Nondo zinavyotengenezwa hatua kwa hatua na hatimaye kupelekwa sokoni kwa kuuzwa,mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  waliotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 

 Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC  wakipewa maelezo namna ya uzalishaji wa Nondo unavyofika
Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies Sailesh Pandit akiwaongoza Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  waliotembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
Meneja wa Kampuni ya  Lodhia Group of Companies, Harminder Bhachu akiwaonesha Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC nondo zikiwa tayari kusafirishwa maeneo mbalimbali kwa matumizi.
 Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  wakiangalia namna mabomba ya Platic yanavyotengenezwa  ndani ya kiwanda cha Lodhia Group of Companies, hatua kwa hatua na hatimaye tayari kwa matumizi
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Toni Filbert akizungumza mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda (hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Lodhia Group of Companies,kilichopo wilayani humo mkoani Pwani.
 

Na Mwandishi Wetu, APC BLOG, PWANI

WAJUMBE wa Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) wametapa nafasi ya kutembelea viwanda 21vinavyofanya  uzalishaji kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Wakiwa katika viwanda hivyo wajumbe hao wamekiri na kuridhishwa na ambavyo Serikali ya Tanzania namna ilivyodhamiria katika Uwekezaji katika viwanda huku wakieleza wazi Tanzania wanayo nafasi kubwa ya kumiliki soko la Jumuiya hiyo kwani kuna kila.kitu zikiwemo malighafi za uhakika.

Baadhi ya wajumbe wa SADC wameiambia Michuzi TV na Michuzi Blog kuwa Tanzania ipo katika nafasi nzuri ya kulimiliki soko la jumuiya hiyo kwa kuwa kuna nguvu kazi ya kutosha na malighafi za uhakika.

Mjumbe kutoka nchini Afrika Kusini wa Kampuni ya Flexion Renatus Joseph amesema kwamba yeye yupo katika sekta ya viwanda vya chuma jijini Johannesburg, Afrika Kusini na kwamba aliyoyashuhudia katika kiwanda cha Lodha Group of Companies yamenifanya abadili fikra zake kuhusu uwezo wa viwanda kwa nchi ya Tanzania.

Amesema amethibitisha kwa macho yake kuna matumizi makubwa ya teknolojia katika utengenezaji bidhaa za nondo na vifaa vingine vitokanavyo na chuma. “Hakika vikipatikana viwanda vingi vya namna hii SADC tutapiga hatua na tutakuwa na bidhaa zinazoleta ushindani ndani na nje ya Afrika,” amesema.

Wajumbe hao wakiwa kiwandani hapo yameelezwa kiwanda hicho cha chuma kilichopo Mkuranga mkoani Pwani ni miongoni mwa viwanda vilivyoitikia mwito wa Rais Dk. John Magufuli kwa vitendo kuhusu Tanzania ya viwanda.

Akizungumza mbele ya ujumbe wa SADC waliotembelea kiwandani hapo Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhandisi Kamara Gombe amesema Tanzania kwa sasa inazalisha tani 200,000 za bidhaa za viwanda huku mahitaji ni tani 300,000.

“Hii maana yake kuna uhaba wa tani laki moja kwenye soko. Hivyo, Kampuni ya Lodhia ni miongoni mwa wadau wa viwanda wanaohakikisha Tanzania inajitegemea katika sekta ya viwanda.Hata hivyo, mbali ya uhitaji huo wa tani laki moja bado kuna tatizo la uhaba wa soko kwa kuwa wanazalisha tani 3000 kwa mwezi

“Lakini uwezo wao ni kuzalisha tani 10,000. Kazi yetu viwanda ni kulinda viwanda vya ndani, tutahakikisha tatizo hili tunalitafutia ufumbuzi ili hizi tani 7,000 zilizobaki ziweze kuzalishwa,” amesema Gombe.

Wakati Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Toni Filbert amesema wilaya hiyo pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla wanazo fursa nyingi za uwekezaji kutokana na ardhi kubwa yenye rutuba. Vilevile, kuna bidhaa nyingi za kimkakati zinazozalishwa na wazawa.

Akitoa maelezo kuhusu uwezo wa kiwanda hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies,Sailesh Pandit alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1996 wakiwa wanafanya biashara ya jumla ya kuuza vyuma ambapo mwaka 2004 ndio walianza kuzalisha vyuma katika kiwanda kilichopo mkoani Arusha.

“Vilevile tuligeukia bidhaa nyingine ikiwemo mabomba ya maji, Gypsum Board, matenki ya ya kuhifadhia maji na bidhaa nyingine za ujenzi kwa kuhakikisha Tanzania ina

jitosheleza katika vifaa vya ujenzi bila kuagiza nje ya nchi,” amesema Pandit na kufafanua wanamshukuru Rais Magufuli kwa kuwahamasisha kuwekeza kwa nguvu na pia amesaidia kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa kila kampuni bila kupendelea.

Mkurugenzi huyo pia aliiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuweka “kodi kinzani” kwa asilimia kati ya 30/40 kwa bidhaa za chuma kutoka nje ili  kuvilinda viwanda vya ndani ambavyo kwa pamoja vina uwezo wa kuzalisha  zaidi ya tani 400,000 kwa mwaka iwapo viwanda hivyo vitafanya kazi kwa asilimia 100.

“kwasasa sisi tunafanya kazi kwa massaa nane tu badala ya masaa 24 na sababu kubwa ni kukosekana kwa soko la ndani la uhakika la bidhaa za chuma kutokana na hatua ya serikali kuruhusu chuma kutoka nje kuingizwa bila ya kulipiwa ushuru hasa kutoka nchi za SADC”alisema Mkurugenzi huyo.

Pandit aliongeza kuwa hatua ya serikali kuweka kodi kinzani italeta manufaa makubwa ya kiuchumi kwa kuongeza ajira kwa watanzania na serikali kuongeza mapato yake.