Jengo jipya la ofisi ya taifa ya mashtaka mkoa wa shinyanga lafunguliwa rasmi kwa niaba ya majengo mengine 9

Naibu katibu mkuu Wizara ya katiba na sheria Dkt.
Khatibu Kazungu akikata utepe leo Jumamos Machi 16,2024 ikiwa ni sehemu ya ufunguzi
rasmi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa niaba
ya majengo mengine tisa (9) ya ofisi za mashtaka za Mikoa.


Na Mapuli Kitina Misalaba

Naibu katibu mkuu Wizara ya katiba na sheria Dkt.
Khatibu Kazungu leo Machi 16,2024 amefungua rasmi jengo jipya la ofisi ya Taifa
ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya majengo mengine tisa (9) ya ofisi za
mashtaka za Mikoa.

Hafla ya ufunguzi huo imehudhuruwa na viongozi
mbalimbali nje na ndani ya Mkoa wa Shinyanga na kwamba jengo hilo lipo katika
eneo la mtaa wa Miti mirefu Manispaa ya Shinyanga.

Katika taarifa yake Mkurugenzi wa mashtaka Nchini
Bwana Sylivester Mwakitalu amesema majengo mengine ya mashtaka yapo katika Mkoa
Mikoa ya Mbeya, Katavi, Rukwa, Pwani, Ilala, Morogoro, Geita, Manyara pamoja na
Njombe.

Amesema ili watumishi waweze kutoa huduma bora kwa
wananchi ni muhimu kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa watumishi
ikiwemo kujenga ofisi zenye majengo bora na vitendea kazi katika Mikoa na
Wilaya zake.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa kutokana na kukamilika
kwa majengo hayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kufikia malengo yaliyokusudiwa
katika utoaji wa huduma bora hasa kwenye eneo la haki jinai.

“Muundo
wa ofisi ya Taifa ya mashtaka unaelekeza kuwepo kwa ofisi za mashtaka Mikoa na
Wilaya zote, hadi sasa zipo ofisi za mashtaka katika Mikoa yote ya kiserikali
pamoja na Mikoa minne ya kimashtaka hivyo kufanya jumla ya ofisi za Mikoa
Thelathini (30) n azote zinafanya kazi”.

“Katika
utekelezaji wa miradi hii mtaalam mwelekezi ni chuo cha Dar es Salaam kwa
miradi kumi ya ofisi za Mikoa kwa thamani ya Shilingi 1,799,000,000 na wakala
wa majengo Tanzania kwa mradi wa ujenzi wa ofisi ya Taifa ya mashtaka makao
makuu kwa gharama ya Shilingi 1,845,000,000”.
amesema Sylivester

Naibu katibu mkuu Wizara ya katiba na sheria Dkt.
Khatibu Kazungu pamoja na mambo mengine amesema ni vema kila mmoja kuhakikisha
anatekeleza majukumu ya ofisi ya Taifa ya mashtaka kwa mujibu wa wa sheria,
kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali iliyopo.

Amesema hatua hiyo itasaidia kuleta maboresho
makubwa katika mnyororo wa utoaji wa huduma ya haki jinai huku akimpongeza Rais
Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushinikiza  suala la haki jinai.

“Ni
matarajio yangu uthubutu wa ofisi katika miradi ya ujenzi kama hii na mambo
mengine utaendelezwa na hivyo kuleta maboresho makubwa katika mnyororo wa
utoaji wa huduma ya haki jinai kwa kusogeza huduma karibu na wananchi na
hatimaye kupata haki kwa wakati”.

“Sote
ni mashahidi kwa kuona na kusikia Rais Samia Suluhu Hassan anavyotilia mkazo
suala la haki jinai ikiwemo kuunda tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha taasisi
ya haki jinai napenda nitumie nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa
nia yake ya dhati ya kuleta mageuzi makubwa katika sekta hii ya haki jinai”.
amesema
Dkt. Kazungu

Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Shinyanga (inajumuisha
Mikoa miwili Shinyanga na Simiyu) Frank Habibu Mahimbali ameipongeza ofisi ya
mashtaka Taifa kwa ubunifu huo wa kujenga ofisi ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga
huku akimiza watumishi wa mashtaka hayo kwa kasi zaidi kwa kuwa tayari
miundombinu ni rafiki.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude naye amempongeza Rais wa awamu ya sita
Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha haki jinai na utawala bora unapewa
nafasi kubwa Nchini huku akisema ofisi hiyo itasaidia kuharakisha upatikanaji
wa haki kwa wananchi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace
Butondo akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya
utawala katiba na sheria amesema ofisi ya mashtaka itaendelea kupewa kipaumbele
katika suala la utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Sisi
watu wa Shinyanga tunayofuraha kubwa sana kuona ujenzi huu wa jengo la Mashtaka
umekamilika lakini  kwa niaba ya kamati ya
kudumu ya Bunge  naomba kutoa salamu kwa
niaba ya Mwenyekiti  kuwa kamati
imefurahishwa sana na imevutiwa sana na usimamizi mzuri wa mkurugenzi wa
Mashtaka Mhe. Mwakitalu hasa kwenye usimamizi wa fedha za miradi”.

“Serikali
inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassani imejikita kuhakikisha kwamba huduma
zinazotolewa na Mahakama zinatolewa katika kiwango bora kwa wakati ili kila
mtanzania anufaike na huduma bora ya kisheria ambayo ni matarajio ya kila
mtanzania kwamba katika haki inayotolewa na sheria ndiyo msingi wa kujenga
amani”
amesema Mbunge wa Kishapu Mhe. Butondo

“Sisi
sote tunafahamu kuwa Bunge linashughulika na kutunga sheria lakini pia hata
masula mazima ya kibajeti ya Serikali yetu muhimili wa Mahakama ni muhimili
ambao sisi kama wabunge tumekuwa tukitoa kipaumbele kwa kadri ambao bajeti za
kwao zinakuja tunawapitishia ili mradi watekeleze miradi yao mbalimbali ya
ujenzi wa Mahakama na tunaona huduma zinavyotolewa vizuri kwa wananchi”.

“Matumaini
yetu ya kamati ya Bunge ya utawala katiba na sheria ni kwamba ubora wa jengo
hili la mashtaka ni matokeo ya utolewaji wa huduma bora kama matumaini ya
watanzania na Bunge kwa ajili ya kutoa huduma bora zilizosahihi  za kisheria, sisi tunakuhakikishia katika
mahitaji mtakayoyahitaji katika ofisi ya mashtaka tutahakikisha inapewa
kipaumbele na hasa katika miradi ya maendeleo
”amesema Mbunge wa
Kishapu Mhe. Butondo
Muonekano wa jengo la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga.

Muonekano wa jengo la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga.Naibu katibu mkuu Wizara ya katiba na sheria Dkt.
Khatibu Kazungu akizungumza katika hafla ya  ufunguzi rasmi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa
ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya majengo mengine tisa (9) ya ofisi za
mashtaka za Mikoa.

Naibu katibu mkuu Wizara ya katiba na sheria Dkt.
Khatibu Kazungu akizungumza katika hafla ya  ufunguzi rasmi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa
ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya majengo mengine tisa (9) ya ofisi za
mashtaka za Mikoa.

Mkurugenzi wa mashtaka Nchini Bwana Sylivester
Mwakitalu akizungumza katika hafla ya  ufunguzi
rasmi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa niaba
ya majengo mengine tisa (9) ya ofisi za mashtaka za Mikoa.

Mkurugenzi wa mashtaka Nchini Bwana Sylivester
Mwakitalu akizungumza katika hafla ya  ufunguzi
rasmi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa niaba
ya majengo mengine tisa (9) ya ofisi za mashtaka za Mikoa.

Kwaya ya AICT Makongoro kutoka Mwanza ikiimba wimbo maalum katika hafla ya ufunfuzi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga.


Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Shinyanga (inajumuisha
Mikoa miwili Shinyanga na Simiyu) Frank Habibu Mahimbali akizungumza leo kwenye
hafla ya ufunguzi wa jengo la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga.

Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Shinyanga (inajumuisha
Mikoa miwili Shinyanga na Simiyu) Frank Habibu Mahimbali akizungumza leo kwenye
hafla ya ufunguzi wa jengo la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga.