Maelfu kujitokeza maandamano chadema

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe akiongoza viongozi wengine wa Kitaifa wakati wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza hutubia maelfu ya Wananchi Jijini Arusha

Egidia Vedasto

Arusha

Maelfu ya watu wamejitokeza katika maandamano yaliyoandaliwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha yaliyoanza asubuhi katika vituo vya TANAPA, Morombo na kwa mrefu na kukutana katika viwanja vya reli vilivyoko jijini Arusha.

Maandamano hayo licha ya mvua kunyesha lakini haikuwa changamoto kwao bali ilikuwa nguvu ya kuchochea safari Yao,  iliyofanya Jiji la Arusha kuwa na vuguvugu za nguvu

Akihutubia Katika mkutano huo Mwanasheria Boniface Mwabukusi amesema maandamano hayo ni hatua kamili ya kupata kinachotakiwa na Watanzania wote.

“Nawapongeza sana kujitokeza na kuvumilia licha ya mvua kubwa zilizonyesha lakini bado mliendelea kwa sababu mnachokitaka ni maisha Bora na upatikanaji wa huduma  za Jamii ambazo bado hazipatikani kutokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichoko madarakani.

” Naendelea kuwatumia Salam na kuwasisitiza wenzetu wa CCM wasirudie kufanya walichokifanya katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 bali tunataka uhuru na haki itendeke katika uchaguzi ujao wa 2025 vinginevyo tutatafuta haki yetu kwa namna yoyote” amesisitiza Mwambukusi.

Wananchi ikiwemo Jamii ya wamasai waliotoka maeneo ya ngorongoro na Mkoa wa Tanga ambako wamasai walihamishiwa na makundi mbalimbali ya watu ikiwemo waendesha bodaboda, wafanya biashara wa biashara ndogondogo wameujaza uwanja wa relini.

Makamu Mwenyekiti Chadema, Tundu Lisu akihutubia

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini Godbless Lema  amesema maandamano ya Leo imetosha  serikali kutambua kuwa wananchi wako tayari kuandamana ili kupata Demokrasia huru na katiba mpya.

Ameongeza kwa kuitaka serikali ya Mkoa wa Arusha kuachana na vikwazo na sababu zisizo za msingi pindi maandamano yanapoitishwa,  kwani maandamano ni ishara  inayoashiria wananchi kuionyesha serikali kuwa wamechoka na wanataka haki.  

“Sauti ya wengi ni Sauti ya Mungu naamini serikali itafanyia kazi kwa hiki kilichofanyika leo” amesema Lema.

Akihutubia umati wa maelfu ya watu waliojumuika katika viwanja vya reli jijini Arusha Mwanasheria Antipas Lisu amesema watanzania wamechoka kwa kutosikilizwa  na serikali iliyopo madarakani hivyo maandamano yataendelea we ili haki ipatikane.

Ameendelea kusema kwamba “Jeshi la polisi nchini linatakiwa  kuwalinda wananchi na sio kuwasonga na kuwagasi kama ambavyo wamefanya Leo wakati maandamano yaliyoanza katika kituo Cha Morombo mapema Leo asubuhi” ameeleza Lisu.

Aidha ameeleza kwamba mfumuko wa bei kwa bidhaa muhimu kama sukari ni hatari kubwa  kwa wananchi wengi wenye Hali ya chini na wenye kipato Cha chini. 

Hata hivyo Lisu  amesema kwamba viongozi wa serikali wanajilimbikizia mali kwa kujinunulia magari ya kifahari kwa kutumia kodi za wananchi badala ya kununua magari ya ya kubeba wagonjwa na kununua vitendanishi vingine.

Akihutubia maelfu ya waandamanaji katika viwanja vya relini jijini Arusha Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema maandamano yatakuwa endelevu Hadi serikali ichukukue hatua kwa kuwafanyia Watanzania wanachostahili.

“Licha ya kutembea kilomita za mraba 30 huku mvua zikinyesha takriban masaa mawili bado watu hawakukubali kusitisha maandamano taswira hii inaashiria Watanzania wanataka mabadiliko na sio kudanganywa kwa siasa za uongo” Amefafanua Mbowe.

Wafuasi wa Chadema wakiwa wameshikilia mabango yenye ujumbe tofauti katika mkutano huo

Akifunga mkutano huo Mbowe amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuacha kufuja kodi za wananchi kusafiri kwenda nje makundi ya watu suala ambalo ni ubadhilifu wa mali za umma na kuwaumiza walipa kodi wanaoishi maisha duni.

“Mimi nashangaa Samia akisafiri unamuona Kikwete pembeni yake kwani Kikwete amekuwa? Mbowe ameuliza, Ametumika miaka yake kumi madarakani anatakiwa akapumzike aache kufuja kodi za wanyonge kwa sababu yeye ana mshahara na ana marupurupu” amesema Mbowe.

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya Wananchi Jijini Arusha

Maandamano hayo yameongozwa na viongozi mbalimbali kutoka bara na visiwani wakiwemo Mwenyekiti Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Naibu Katibu Mkuu CHADEMA zanzibar Salum Mwalimu, Mwenyekiti Kanda ya ya Kaskazini Lema ambaye alikuwa mwenyeji wa maandamano hayo, Mwanasheria Lisu, Heche, Sugu, Msigwa, na wengine wengi.

Mwenyekiti CHADEMA Kanda ya Kaskazini Godbless Lema_
_Maelfu ya wananchi wakisikilizakwa makini hotuba kutoka kwa viongozi wa Chama Cha CHADEMA_