MCHANGO WA CSO KATIKA JAMII UMEENDELEA KUZAA MATUNDA

Egidia Vedasto

APC Media, Arusha.

Umoja wa Asasi za Kiraia Nchini zimekuwa mchango mkubwa wa kuchochea maendeleo na kubadilisha maisha ya watu wengi nchini ikiwemo makundi maalum, wanawake na watoto.

Akizungumza wakati wa kufunga Wiki ya CSO Jijini Arusha, Meneja Mradi wa Kusaidia Watoto Tanzania Nemes Temba, amesema mchango wa Asasi za Kiraia ni mkubwa na zimebadilisha jamii kwa upana.

“Wakati nazaliwa hakukuwa na mwanga juu ya watu wenye ulemavu, jamii ilikuwa na mawazo potofu kwa mtoto anayezaliwa na ulemavu, lakini leo historia imebadilika, tumeaminika na tunaweza kuongoza jamii”

“Natamani uchaguzi mkuu ujao Watu wenye Ulemavu wawe miongoni mwa wagombea, naomba mtuamini na kutuchagua sababu tunaweza kubadilisha jamii katika masuala ya maendeleo” amesema Temba.

Pia Mkuu wa Biashara Incubator Benki ya Stanbic Tanzania Kai Mollel, amewataka vijana kuwa wabunifu, kuchangamkia fursa zilizopo na kuzingatia maadili na nidhamu katika harakti zao za kujikwamua na umasikini.

“Tanzania tuitakayo inategemea nidhamu na kujituma, namna tunavyochukulia mambo muhimu katika harakati za kujikwamua na umasikini, Katika jitihada za CSO vijana tutumie teknolojia kuongeza kipato na kuacha malalamiko yasiyo ya lazima” ameshauri Mollel.

Hata hivyo amewataka Vijana kujifunza kwa Mababu zetu, kuhusu maadili, ambao walifanikiwa kudumisha umoja, ushirikiano na upendo katika kipindi chao, hatua iliyosaidia tukawakuta kwenye hatua nzuri, ambayo kuna vitu vingi vya kujifunza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya AZAKI CPA. Mercy Sila katika hotuba yake, amesema Mkutano huu umejumuisha washiriki takriban 900 kutoka nchi nzima, ambapo Mashirika mbalimbali yamewasilisha mada zilizoibua na kuchagiza maendeleo na mabadiliko katika jamii.

Mada zilizowasilishwa ni pamoja na Utoaji Maoni Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Ulinzi wa Mtoto, Uchumi na Maendeleo ya Mwanamke, Mikakati ya kupambana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi, Uongozi na Utawala na nyingine nyingi.

Washiriki wa Wiki ya CSO Jijini Arusha

“Sisi CSO huwa tunakutana kila mwaka kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa mipango iliyopita na kuweka mikakati mipya ya namna ya kufanya kazi, kuweka mipango mikakati namna ya kufanya kazi pamoja” ameeleza CPA. Sila.

Pia Rais wa Mahakama ya Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Jaji Iman Abood, amehimiza mkakati endelevu wa ulinzi wa mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabianchi ili Kizazi cha miaka ijayo kinufaike na uoto wa asili ulioachwa na Mababu zetu.

Aidha amesema kwamba utekelezaji wa sera kwa ufanisi na ushirikishwaji utawanufaisha wananchi na kuchochea maendeleo yao.

“Sisi Jumuiya za Kiraia tunaendelea na juhudi za utetezi kwa kushirikiana na serikali na sekta binafsi kuwezesha jamii kuchukua umiliki wa maendeleo yao” ameeleza Jaji Aboud.

“Sisi Jumuiya za Kiraia tunaendelea na juhudi za utetezi kwa kushirikiana na serikali na sekta binafsi kuwezesha jamii kuchukua umiliki wa maendeleo yao” ameeleza Jaji Aboud.

Meneja Mradi wa Kusaidia Watoto Tanzania Nemes Temba