Mstahiki meya masumbuko aelekeza matangazo ya zabuni kuwekwa wazi

Na Moshi Ndugulile

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Elius Ramadhan Masumbuko  kwa kushirikiana na serikali kuu imeendelea kubaini
maeneo yenye uhitaji wa kujengwa Shule za Msingi na sekondari, kama hatua ya
kuondoa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata masomo

Hayo yameelezwa na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius kagunze,kwenye kikao cha Baraza la madiwani ,wakati akijibu
swali lililoulizwa na Diwani wa kata ya koladoto Mheshimiwa Mussa Elias aliyetaka kujua mkakati wa
serikali kujenga shule katika kijiji cha Galamba ili kuondoa changamoto ya
wanafunzi kutembea umbali mrefu

Kagunze amesema ili
kuondoa changamoto hiyo serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi mbali mbali ikihusisha sekta ya Elimu

Halmashauri ya Manispaa
ya Shinyanga kwa kushirikiana na serikali kuu imeendelea kubaini maeneo yenye
uhitaji wa kujengwa Shule za Msingi na sekondari, kama hatua ya kuondoa
changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata masomo

Hayo yameelezwa na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius kagunze,kwenye kikao cha Baraza la madiwani ,wakati akijibu
swali lililoulizwa na Diwani wa kata ya koladoto Mheshimiwa Mussa Elias aliyetaka kujua mkakati wa
serikali kujenga shule katika kijiji cha Galamba ili kuondoa changamoto ya
wanafunzi kutembea umbali mrefu

Kagunze amesema ili
kuondoa changamoto hiyo serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi mbali mbali ikihusisha sekta ya Elimu

matangazo ya zabuni 
zote, ili kutoa nafasi  kwa
Wananchi wote kutumia fursa hizo

Ametoa maelekezo hayo jana kwenye kikao cha baraza la
Madiwani wa Halmahauri ya Manispaa ya Shinyanga,kilichofanyika kwenye ukumbi wa
Lews kalinjuna Mjini Shinyanga

Meya huyo amesisitiza kuwa matangazo yote ya zabuni yawekwe
wazi kwenye maeneo yote ya wazi ikiwemo kubandikwa kwenye mbao za matangazo
katika ofisi za maafisa watendaji wa kata, ili wananchi wapate nafasi ya kusoma
na kutumia fursa hiyo.

Wakati huo huo Mstahiki Meya amewataka   Madiwani kuendelea kushirikiana na na
watumishi wa halmashauri wakiwemo wataalamu na watendaji wengine katika hatua
za kusukuma maendeleo na ustawi wa wananchi.

“Lakini katika baadhi ya maeneo
watendaji wanataka usirikiano na Madiwani,sasa kuna mahali wanakutana na
changamoto za kiutendaji waaoingia kwenye shughuli za uwajibikaji,kwamba wapiga
kura wangu waachwe,sasa waache kwa sababu zipi ?naomba tuangalie shughuli za
serikali na shughuli zetu kama wawakilishi,tuwape nafasi watendaji wafanye
shughuli zao,hapa tumeona kuna miradi mingi ambayo tunasema itekelezwe,nah ii
miradi inahitaji mapato,sasa kama tunasema watendaji wasiwaingilie wananchi,kwa
sababu ya kigezo cha uchaguzi manake hata hiyo miradi haiwezi kutekelezeka,manake
itekelezeke  baada ya Uchaguzi,na sisi
mikakati yetu ipo kwenye mpango wa utekelezaji,kwa hiyo naomba tuwape
ushirikiano,sasa tusimamie mambo haya,tusiwape wakati mgumu wa kufanya kazi
zao,kwani na wao wana wajibu wa kutoa taarifa za utekelezaji kwa mamlaka
zinazowatuma”amesema Mstahiki Meya.

Wakati huo huo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze amesema Halmashauri
hiyo kwa kushirikiana na serikali kuu imeendelea kubaini maeneo yenye uhitaji
wa kujengwa Shule za Msingi na sekondari, kama hatua ya kuondoa changamoto ya
wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata masomo

Ametoa kauli hiyo wakati
akijibu swali lililoulizwa na Diwani wa kata ya koladoto Mheshimiwa Mussa Elias aliyetaka kujua mkakati wa
serikali kujenga shule katika kijiji cha Galamba ili kuondoa changamoto ya
wanafunzi kutembea umbali mrefu,

Kagunze amesema ili
kuondoa changamoto hiyo serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi mbali mbali ikihusisha sekta ya Elimu

“Serikali
imeendelea kutuma fedha kwa ajili ya shule au miradi mbali mbali ambapo katika
eneo hilo walipita wataalamu kutoka katika wizara ofisi ya Rais TAMISEMI na
kubainisha maeneo ambayo yalionekana kwamba yatafaa kuongezewa shuleili
kupunguza wanafunzi waliojaa katika shule moja lakini kuondoa changamoto ya
umbali,na mfano mzuri ni shule ya 
Sekondari Ngokolo B, (Siyo jina rasmi)ambayo imeletewa fedha shilingi
Milioni 603,lengo ni kupunguza idadi ya wanafunzi.

Mategemeo
yetu ni kufanya ufuatiliaji kutoka serikalini ili kuona kama watatupatia fedha
kwa sababu eneo lililotajwa wanafunzi wanatoka mbali”ameeleza Mkurugenzi huyo.

Katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani,waheshimiwa hao
wamewasilisha taarifa za utekelezaji ambapo pamoja na kubainisha
mafanikio,wametaja pia changamoto zilizopo katika kata zao.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Bwana Anold Makombe
amepongeza juhudi za Madiwani kwa kushirikiana na Mkurugenzi pamoja na
watumishi wa Halmashauri katika utekelezaji wa miradi  hali inayochochea maendeleo na ustawi wa
wananchi.

 

Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga (aliyesimama) akizungumza kwenye kikao cha Baraza la madiwani.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga  Mwalimu Alexius Kagunze akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani .
Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kikiendeleo katika ukumbi wa Lewis Kalinjuma..