Meya wa manispaa ya shinyanga mhe. masumbuko atembelea chuo cha serikali za mitaa kampasi ya shinyanga asisitiza umuhimu wa elimu

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga  Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amewataka
wanafunzi katika chuo cha serikali za mitaa kampasi ya Shinyanga kujielekeza
kwenye elimu ili waweze kutimiza ndoto zao.

Ameyasema hayo Alhamis Oktoba 26,2023 baada ya kufanya ziara ya siku
moja ya kutembelea chuo hicho ambapo amewasisitiza wanafunzi hao kutojihusisha na
makundi ya wahalifu na badala yake wasome kwa bidii ili kufikia malengo
waliyojiwekea.

Mstahiki meya Mhe. Masumbuko amesema ni muhimu wanafunzi hao
kujielekeza kwenye elimu kwa kuhakikisha wanasoma kwa bidii, na nidhamu ikiwa
ni pamoja na kuzingaia sheria na taratibu zilizopo.

“Ni imani yangu kubwa sana kama mtazingatia
haya ambayo mmeijia hapa chuoni naamini kabisa hamtatoka kama mlivyo mtatoka
mmepata elimu ya kutosha ambayo inakufanya uende kutumika moja kwa moja kikubwa
sana ni nidhamu kama huna nidhamu huwezi kuzingatia kile ambacho kimekufanya
utoke huko unakoishi uje hapa kwa sababu ukikosa nidhamu utatengeneza mazingira
ya nidhamu yako yakutokuwa na uoga kwa wale wanaokusimamia na hata huko nje
mnakoishi mtaendelea kukutana na watu wenye tabia tofauti ebu mjielekeze tu
ninyi kwamba mmekuja kutafuta elimu nasivinginevvyo”.amesema Mhe. Masumbuko

Mhe. Masumbuko ametumia nafasi hiyo kuipongeza serikali ya awamu ya
sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha jambo hilo
la kuleta chuo cha serikali za mitaa katika Mkoa wa Shinyanga.

Mstahiki meya huyo Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amewahakikishia
wanafunzi na walimu katika chuo hicho cha serikali za mitaa kuendelea kutoa
ushirikiano wake katika shughuli mbalimbali za kuchochea maendeleo.

Kwa upande wake mkuu wa chuo Cha serikali za mitaa kampasi ya
Shinyanga  Dkt. Kasubi amewasihi
wanafunzi hao kutokata tamaa na mwamba wanapaswa kuwa wavumilivu ili waweze
kuhitimu salama.

Amewasisitiza wanafunzi hao kuendelea kuzingatia yale yote
wanayokubushwa na viongozi mbalimbali wa serikali ili waweze kufikia malengo
waliyojiwekea.

Baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wamesema wataendelea kuzingatia
Sheria na taratibu zilizopo ili waweze kufikia malengo yao.

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga  Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akiwasisitiza
wanafunzi wa chuo cha serikali za mitaa kampasi ya Shinyanga kusoma kwa bidii
ili waweze kutimiza ndoto zao, baada ya kuwatembelea leo Alhamis Oktoba
26,2023.

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga  Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akiwasisitiza
wanafunzi wa chuo cha serikali za mitaa kampasi ya Shinyanga kusoma kwa bidii
ili waweze kutimiza ndoto zao, baada ya kuwatembelea leo Alhamis Oktoba
26,2023.

Wanafunzi wa chuo cha serikali za mitaa kampasi ya Shinyanga wakiwa
katika hafla hiyo leo Alhamis Oktoba 26,2023.