Na Mapuli
Misalaba, Shinyanga
Jumla ya wanafunzi
74,746 Mkoani Shinyanga kati yao
wasichana ni 38,800 na wavulana 35,946 leo
Oktoba 26,2023 wanatarajiwa kumaliza mtihani wa kujipima wa Darasa la Nne SFNA.
Akitoa takwimu hizo
Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Shinyanga Bi.
Fausta Luoga amesema kati ya wanafunzi
hao 72,197 ni watahiniwa wa shule za serikali huku 2, 549 ni shule binafsi.
Afisa Elimu huyo
amefafanua kuwa watahiniwa wa shule za serikali wasichana ni 37,519 na wavulana
ni 34, 678 wakati shule binafsi wasichana ni 1281 na wavulana ni 1268.
Afisa Elimu huyo
ametumia nafasi hiyo kuwataka wasimamizi wa mitihani hiyo ambayo imeanza jana
Oktoba 25.2023, kuzingatia kanuni na taratibu za usimamizi wa mitihani ikiwa ni
pamoja na kujiepusha na udanganyifu wa aina yeyote.
Amewakumbusha wazazi
kuchochea ari ya wanafunzi hao kufanya vizuri mitihano yao na kuepuka kuwa
chanzo cha kuwakatisha tamaa.
Baadhi ya wanafunzi katika Manispaa ya Shinyanga wameahidi kufanya
vizuri katika mitihani hiyo inayomalizika leo Oktoba 26 2023.