Mwanamke mkazi wa kata ya masengwa halmashauri ya wilaya ya shinyanga amefariki dunia baada ya kunywa sumu ya panya.

Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga

Mwanamke anayefahamika
kwa jina la Naomi Zengo anayekadiriwa kuwa na umri wa Miaka 30 mkazi wa
Kitongoji cha Ilebelo kijiji cha Ilobashi kata ya Masengwa Halmashauri ya
Wilaya ya Shinyanga amefariki Dunia baada ya kunywa sumu.

Kwa mujibu wa
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ilebelo Bwana Elius
Jitilu
amesema tukio hilo limetokea Oktoba 22,2023 majira ya saa tano
asubuhi ambapo mwanamke huyo alikunywa sumu ya panya.

Amesema baada ya
kupokea taarifa hizo  walichukua hatua za
haraka kumpeleka katika Zahanati ya kijiji kwa ajili ya matibabu ambapo alipata
huduma ya kwanza na kisha kupewa rufaa kwenda Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga.

Mmoja wa watu
walioshuhudia tukio hilo ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema kabla ya
kunywa sumu mama huyo aliwaambia baadhi ya majirani na wanafamilia kwamba
atakunywa sumu ili afe kwa sababu ya maumivu ya mume wake kuoa mke wa pili.

Inaelezwa kuwa mume wa
marehemu huyo alikuwa na siku chache akiwa ameoa mke wa pili.