Ajali ya moto katika mtaa wa mwasele b kata ya kambarege manispaa ya shinyanga

Kamanda wa Jeshi la
Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga Mrakibu Martin Nyambala ametoa wito kwa wazazi
na walezi kuwajibikia suala la ulinzi na usimamizi kwa watoto wanapokuwa
nyumbani ili kuepukana na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza ikiwemo
ajali za moto.

Ametoa wito huo  wakati akizungumza kufuatia ajali ya moto iliyotokea Oktoba 20,2023 majira ya saa sita mchana katika Mtaa wa Mwasele B Kata ya Kambarege Manispaa
ya Shinyanga na kuteketeza nyumba ya Bwana Rojaz Pius.

Kamanda huyo amesema taarifa
za awali zimeonesha kuwa moto huo umesababishwa na mtoto aliyekuwa akicheza
ndani ya nyumba hiyo lakini Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini
ukweli wa chanzo cha tukio hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Mtaa huo Bwana Cosmas Lukas ameeleza namna alivyopokea taarifa za tukio hilo
na hatua mbalimbali zilizochukuliwa kunusuru mali na wakazi wa familia hiyo.

Nao baadhi ya majirani
walioshuhudia tukio hilo wamepongeza hatua mbalimbali zilizochukuliwa na
wananchi kwa kushirikliana na Jeshi la Zimamoto na uokoaji pamoja na Shirika la
Umeme Tanzania TANESCO kudhibiti moto huo.