Na Mapuli Misalaba -Shinyanga.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM U.W.T Wilaya ya Shinyanga Mjini Bi Rehema Nhemanilo
amewaagiza Madiwani wanawake wa kata na viti Maalumu wa Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga kutafuta ufumbuzi wa Changamoto zilizopo katika kituo cha makazi salama ya wasichana wahanga wa ukatili ,ndoa na mimba za
utotoni kinachomilikiwa na shirika la
Agape Aids Control program katika Manispaa ya Shinyanga.
Nhemanilo ametoa agizo hilo leo wakati Wajumbe wa kamati ya
utekelezaji ya Umoja wa Wanawake wa CCM
U.W.T Wilaya ya Shinyanga Mjini walipotembelea katika kituo hicho kilichopo
katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya
wiki ya U.W.T , ambapo Wilaya ya Shinyanga Mjini imeadhimisha kwa kushiriki
katika shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo kupanda miti na kutembelea
wahitaji
Baada ya kutembelea kituo
cha makazi salama ya wasichana wahanga wa ukatili ,ndoa na mimba za
utotoni Wajumbe hao wa kamati ya
Utekelezaji wakiongozwa na Mwenyekiti Rehema Nhemanilo wamebaini kuwepo kwa changamoto
mbali mbali ikiwemo upungufu wa Chakula,Bima za Afya kwa watoto,upungufu wa
miundo mbinu ya hostel na Madarasa,Deni la Maji
wanalodaiwa na SHUWASA la shilingi
Milioni 6.3.
Nhemanilo amewataka madiwani hao kuchukua hatua za haraka kutafuta
ufumbuzi wa changamoto hizo ambazo zimekuwa kikwazo katika ustawi wa kituo
hicho cha watoto wa kike wahanga wa ukatili ,ndoa na mimba za utotoni kinachomilikiwa na shirika la Agape Aids Control
program katika Manispaa ya Shinyanga.
“ nawaagiza Madiwani wanawake
wa kata na viti Maalumu chukueni hatua za haraka kufuatilia na kupata ufumbuzi
wa Changamoto zinazokikabili kituo cha Agape, ili Watoto hawa waendelee kupata
huduma zote muhimu”
Awali akizungumza na watoto hao wa kike Naibu Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Diwani wa kata ya Ndala Mheshimiwa
Zamda Shaaban amewaasa wasichana hao kuwekeza zaidi kwenye Elimu ili waweze
kukabiliana na soko la elimu na ajira
Katika risala yao watoto hao wa Agape knowledge Open School
pamoja na kubainisha mafanikio mbali mbali yaliyofikiwa na kituo hicho cha
makazi salama ya wasichana wahanga wa
ukatili ,ndoa na mimba za utotoni ,wametaja changamoto kadhaa ambazo zinahitaji
juhudi za pamoja kuzipatia ufumbuzi,ambapo wameomba wadau ikiwemo U.W.T
kusaidia msaada wa chakula kwa kuwa sirika halina ufadhili wowote na kwamba
halipati ruzuku kutoka serikalini.
Changamoto nyingine kubwa waliyoibainisha kupitia risala hiyo
ni deni la shilingi Milioni 6.3 wanalodaiwa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa
mazingira Shinyanga SHUWASA ( la kuunganishiwa huduma ya Maji) ambalo
limesababisha kusitishiwa huduma ya maji na kufikishwa Mahakamani.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha makazi salama ya wasichana wahanga wa ukatili ,ndoa na mimba za
utotoni cha Agape Aids Control
program Bwana John Myola amewaomba wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya
umoja wa wanawake wa CCM U.W.T Wilaya ya
Shinyanga Mjini kusaidia kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizopo katika kituo
hicho ikiwemo deni kubwa la Shilingi Milioni
6.3 wanalodaiwa na SHUWASA.
Bwana Myola amebainisha kuwa takribani Watoto 4,300 wamepata
malezi na elimu ya ufundi katika vyuo vya VETA na Vyuo vya Maendeleo ya
wananchi FDC, AGAPE Training centre na
SHYNET
Ameeleza zaidi kuwa watoto wapatao 327 wamefanikiwa kupata
elimu ya sekondari kupitia shule ya Agape knowledge Open School ali inayowapa
nafasi ya kuingia kwenye soko la ushindani wa elimu na ajira,huku watoto 27
wamefanikiwa kujiunga na vyuo vikuu vya Tanzania katika fani mbalimbali.
Madiwani wa viti maalumu Zuhura Waziri na Esther Makune,pamoja
na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Bi Juliana
Buzuruga wametumia nafasi hiyo kuwahamasisha vijana hao wa kike kutumia nafasi
hiyo kuweka bidii,juhudi na maarifa
katika masomo ili waweze kuwa kielelezo na mfano thabiti wa ushindi dhidi ya changamoto walizokutana nazo.
Katibu wa U.W.T Wilaya ya Shinyanga Mjini Bi Sharifa Hassan
Mdee ameeleza malengo ya ziara hiyo kuwa ni kuadhimisha wiki ya U.W.T ngazi ya
Wilaya ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe wa kamati ya Utekelezaji U.W.T
Wilaya ya Shinyanga Mjini wameshiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo kufanya
usafi wa mazingira katika baadhi ya taasisi za Umma, kupanda miti na kufanya
usafi katika eneo la ujenzi wa nyumba ya katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga
Mjini iliyopo katika kata ya kitangili
Wajumbe hao wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini ambao pia
walijumuika na Madiwani wa viti Maalumu wakiongozwa na Mwenyekiti Rehema
Nhamanilo, wametoa msaada wa vitu mbali mbali kwa watoto hao ikiwemo taulo za kike,juice,sabuni
za Mche na Unga na mafuta ya kupaka.Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo akisalimiana na viongozi baada ya kuwasili katika kata ya Kitangili ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya umoja wa wanawake wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.
ya wasichana wahanga wa ukatili ,ndoa na
mimba za utotoni kinachomilikiwa na
shirika la Agape Aids Control program katika Manispaa ya Shinyanga.
ya wasichana wahanga wa ukatili ,ndoa na
mimba za utotoni cha Agape Aids Control program Bwana John Myola akiwaongoza viongozi hao kutembelea eneo la kituo hicho.
Mkurugenzi wa kituo cha makazi salama
ya wasichana wahanga wa ukatili ,ndoa na
mimba za utotoni cha Agape Aids Control program Bwana John Myola akiwakaribisha viongozi wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini.