Uvccm arusha wamvaa gambo,kauli ya kikokotoo yamponza, wamtaka akanushe kauli yake dhidi ya rais samia

Ibrahim Kijanga, Katibu wa UVCCM Arusha

Na Mwandishi Wetu, Arusha 

Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha kupitia kwa Katibu wake Ibrahim janga , kimemtaka Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo (CCM) kutengua kauli yake aliyodai kuwa imejaa dhihaka dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan dhidi ya viongozi anaowateua au atoke ndani ya Chama hicho.

“Sisi kama umoja wa vijana mkoa wa Arusha tunakishauri chama chetu ni wakati muafaka wa kuchukua hatua dhidi ya mbunge huyu na kama anaona anabanwa chama  kimruhusu atoke”


Kijanga amesema Gambo amekosa nidhamu na kwa muda mrefu amekuwa kirusi ndani ya chama kutokana na kauli zake tata anazozitoa dhidi ya wateule wa Rais akiwalenga viongozi wa mkoa wa Arusha .

Akizungumzia kauli ambayo Gambo ameitoa hivi karibuni katika mkutano wa wakuu wa shule za sekondari katika shule ya sekondari Arusha, Kijanga amesema Gambo amekosa nidhamu kwa kutoa maneno ambayo yamekifedhehesha chama hicho .

Maneno yanayodaiwa kusemwa na Gambo ni kwamba kazi ya Mbunge ni kuwatumikia wananchi ila kazi ya wateule wa Rais ni kumfurahisha aliyewateua,” alinukuu kijanga.

Amesema ukiangalia maneno hayo ya Gambo ni dhihaka dhidi ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na viongozi wote wateule wa Rais ikiwemo Waziri Mkuu.

“Pamoja na mambo mengine Gambo alizungumza maneno yaliyojaa dhihaka kwa mh Rais lakini pia kwa wateule wa Rais katika mkoa wa Arusha, Maneno yale kama umoja wa vijana yametufedhehesha ndio maana tukasema tuje kuongea na waandishi wa habari”

“Kama ataendelea na tabia hiyo tunafikiria kutoa mapendelezo kwa wakuu wa chama”

“Naamini Gambo alikuwa Dc na baadaye aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa ina maana alikuja kuimba mapambio sisi tunaamini kwamba wateule wote walioletwa na mh Rais wanakuja kuwatumikia watanzania”

“Wateule wote wa Mkoa wa Arusha walioletwa na mh Rais na mwenyekiti wa ccm wameletwa kuja kuwatumikia watanzania na wanafanyakazi nzuri kama zipo changamoto raia huwa anaziona”

“Sisi kama viongozi wa uvccm tunamkemea kwa ukali ache hizo tabia za kifedhuli  tunamtaka ache hizo tabia za kejeli kwa wateule wa rais na ajifunze lugha za staha na ajifunze tamaduni za kuongea na kama hataki atoke ndani ya ccm”

“Hizi ni kauli za kejeli, kauli za dhihaka kauli za dharau aziache na kusema watanzania wanaminywa hawana uhuru serikali inatumia mabavu aiache serikali ya Rais Samia inafanya kazi nzuri sana”

“Sisi kama umoja wa vijana mkoa wa Arusha tunakishauri chama chetu ni wakati mwafaka wa kuchukua hatua dhidi ya mbunge huyu na kama anaona anabanwa chama  kimruhusu atoke”