Kajala wa uwt shinyanga mjini aibuka mshindi uchaguzi

Na Moshi Ndugulile

Wajumbe wa Mkutano Mkuu Umoja
wa wanawake wa CCM, UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, wamemchagua Bi Mariam kajala
kuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya kupitia uchaguzi mdogo wa  kuziba nafasi iliyokuwa wazi

Akitangaza matokeo  hayo msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo Mjumbe wa
Baraza la UWT Taifa Christina Gule amemtaja Bi kajala kuwa mshindi wa nafasi
hiyo baada ya kupata kura 32 kati ya 54 
akiwaongoza wagombea wengine watatu

 Gule amewatangaza wagombea
wengine waliokuwa wakiwania nafasi hiyo kuwa ni pamoja na Mery Izengo ambaye
amepata kura 22,Mary Nzuku hakupata kura,na Theonestina  Martine ambaye pia hakupata kura yoyote

Baada ya kutangaza matokeo hayo
msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo Mjumbe wa Baraza la UWT Taifa Bi Christina Gule
amemtaka kiongozi aliyechaguliwa Bi Mariam kajala kuitumikia kwa uadilifu
nafasi hiyo,na kuhakikisha anakuwa kiungo na chachu ya kuchochea  ushirikiano,umoja na mshikamano baina ya
Wanachama na viongozi wa Chama na jumuiya zake.

 Akizungumza baada ya kutangazwa
mshindi,Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Bi Mariam
kajala, ameahidi ushirikiano zaidi na kwamba atakitumikia Chama na jumuiya zake
uadilifu mkubwa

 Amewaomba wagombea wengine
ambao kura hazikutosha kupata nafasi hiyo, kutokata tamaa na badala yake
waendelee kushirikiana na Chama na jumuiya zake ili kuleta tija na ufanisi

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa
UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Bi Rehema Nhamanilo amesema baada ya Uchaguzi huo
mdogo wajumbe wote wa jumuiya hiyo wanapaswa kuvunja makundi yaliyokuwepo ili
kuendelea na majukumu ya kawaida katika 
kukijenga na kukiimarisha Chama na jumuiya zake zote

 Naye kaimu katibu wa UWT Wilaya
ya Shinyanga Mjini Naibu katalambula ambaye ni katibu wa UVCCM Wilaya ya
Shinyanga Mjini, amewapongeza wajumbe wa Mkutano huo pamoja na
viongozi wote walioshiriki katika Uchaguzi huo mdogo,ambapo amesema demokrasia
imechukua nafasi yake,kwa kuwa Uchaguzi umefanyika katika mazingira ya
uwazi,usawa na haki,huku akisisitiza kuhusu wajibu wa kuendelea kushirikiana

 Uchaguzi huo uliofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini,pamoja na wajumbe wa
Mkutano huo lakini pia ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa
serikali,Chama  na jumuiya akiwemo Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi,Mwenyekiti wa UWT Mkoa Bi Grace Samwel
Bizulu, katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Asha kitandala, na Mary Mpazi Mjumbe wa
Baraza la UWT Mkoa.

  

Mariam Kajala Mjumbe wa Halmasauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini  (akiwakilisha UWT).



Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo akizungumza baada ya uchaguzi


Katibu wa UVCCkatibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini

Mjumbe wa baraza la UWT Wilaya ya Shinyanga mjini  Mary Izengo ambaye alikuwa mgombea 
Matha Nzuku ambaye alikuwa mgombea akiomba kura

Mgombea Theonestina Martine akiomba kura kwa wajumbe
 Viongozi wa UWT Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wagombea
Wajumbe na wagombea wakiburudika baada ya uchaguzi kuisha 



Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT Wilaya ya Shy Mjini
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT Wilaya ya Sinyanga Mjini

 
Viongozi wa UWT mkoa na wilaya wakiwa kwenye picha ya pamoja na wagombea
Viongozi wa UWT mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wagombea na viongozi mbalimbali wa kata 
Viongozi wa UWT mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wagombea na viongozi mbalimbali wa kata 
Viongozi wa UWT mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wagombea na viongozi mbalimbali wa kata 
 
Wajumbe wa kikao cha baraza wakiwa kwenye kikao cha uchaguzi mdogo