Wamasai ngorongoro watoa ombi kwa rais samia.

 Na Mwandhisi wetu-Ngorongoro

Akisoma tamko lao la pamoja la wakazi waishio ndani ya mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, Lengai Ngoishiye amesema wapo tayari kuhama na wanaunga mkono uamuzi wa serikali kuhamia Msomera na maeneo mengine.

Wameiomba serikali ifanye haraka kuwahamisha ili waondokane  na changamoto zinazowakabili ikiwemo kujeruhiwa na kuuawa na wanyama wakali,kukosa uhuru wa kumiliki ardhi na vyombo vya moto,kukosa fursa za maendeleo,kukosa huduma muhimu za kijamii na kutokuwa na makazi bora na ya kudumu.

Aidha wameiomba serikali iwachukulie hatua kali za kisheria wote wanaopotosha na kujaribu kukwamisha zoezi la uhamisho kwa maslahi yao binafsi na kuwachonganisha na serikali yenye dhamira njema kwao waishio ndani ya hifadhi.

Zoezi la kuhama kutoka Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ni la hiari na kila mmoja anaruhusiwa kuhamia popote anapotaka kwa gharama za serikali.