Jeshi la polisi shinyanga lakamata vitu na vielelezo mbalimbali vya wizi

Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga

Jeshi la Polisi Mkoa wa
Shinyanga limekamata vitu mbali mbali vya wizi ikiwemo Mawe yenye madini ya
dhahabu uzito wa gram 6753.2 yenye thamani ya shilingi Bilioni 9.2, katika
mgodi wa Bulyankulu Wilayani kahama Mkoani Shinyanga.

Katika taarifa yake leo Jumatano
Agosti 23,2023 kwa vyombo vya habari kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa
Shinyanga,kamishina msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amesema vitu pamoja na
vielelezo hivyo vimekamatwa kufuatia msako mkali uliofanya na askari wa jeshi
hilo katika kipindi cha Julai na Augusti Mwaka huu.

Amevitaja vitu
vilivyokamatwa kuwa ni pamoja na mawe yenye madini ya dhahabu,carbon yenye
madini yanayodhaniwa kuwa ni dhahabu,Bunduki aina ya raifo,Mafuta aina ya disel ambavyo vilikutwa katika maeneo tofauti
ya Mkoa wa Shinyanga.

“Tumekamata
lita 603 za mafuta aina ya Diesel katika maeneo tofauti ya mradi wa Reli ya
mwendokasi SGR, pia tumefanikiwa kukamata mawe yenye madini ya Dhahabu yenye
uzito wa gramu 6753.4 na thamani ta Shilingi 9,213,116.83/= huko katika mradi
wa machimbo ya dhahabu ya Bulyanhulu lakini pia tumekamata Carbon yenye mchanga
wenye madini yadhaniwayo kuwa ni dhahabu yenye uzito wa Kg 261 ambayo thamani
yake bado haijajulikana huko maeneo ya Manzese Kahama.

Aidha
katika misako hiyo tumefanikiwa kukamata Bunduki aina ya Riffle yenye namba
2/29pf78701 ambayo ilikuwa inatumika katika shughuli za ulinzi bila kibali, pia
tumekamata madawa ya kulevya aina ya Bangi yenye uzito wa Kg 71, seti moja  ya Computer, Pikipiki tatu, Tiles Box 14,
mabomba sita ya chuma na vipande tisa, mabati 17, Plastick tatu za rangi ya
majumba, vipodozi vinavyoaminika kuwa ni sumu tayari jumla ya watuhumiwa 31
wanashikiliwa katika vituo mbalimbali vya polisi kuhusiana na makossa hayo na
wengine wamepewa dhamana huku wakisubiri kufikishwa  Mahakamani”.
amesema
Kamanda Magomi

Kamanda Magomi amesema
katika Msako huo Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 31 wanaosadikiwa
kuhusika na wizi wa mali na vielelezo vilivyokamatwa, ambao wanashikiliwa
katika vituo mbali mbali Mkoani Shinyanga.

Ameeleza pia kwamba kesi
mbalimbali zilizofikishwa mahakamani na jeshi hilo washitakiwa wamepata adhabu
mbali mbali ikiwemo hukumu ya vifungo jela, na wengine kulipa faini.

“Kwa
upande wa mafanikio Mahakamani jumla ya kesi 34 zilipata mafanikio Mahakamani
lakini upande wa usalama barabarani jumla ya makossa 4017 yalikamatwa”.

“Jeshi
la Polisi Mkoa wa Shinyanga linapenda kuwaasa wananchi wote kwa ujumla kufuata
sheria za Nchi na pia kutoa ushirikiano kwa jeshi ili kudumisha amani na
utulivu uliopo”.amesema kamanda Magomi

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga  kamishana msaidizi wa polisi  Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Agosti 23,2023.

 Mwonekano wa vitu mbalimbali vilivyokamatwa na jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kupitia misako iliyofanyika kuanzia Mwezi Julai hadi Agosti 22 Mwaka huu 2023.