minane iliyotembelewa, kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, anaripoti Respice Swetu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mwenge huo kati ya
halmashaurti ya wilaya ya Kasulu na mji wa Kasulu kwenye eneo la Nyumbigwa
mjini Kasulu, kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2023 Abdallah
Kaim, ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Kasulu kwa kazi nzuri ya kusimamia
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopitiwa na mwenge huo na
kuifanya halmashauri hiyo kukamilisha mbio na hati safi.
“Nichukue nafasi hii kumpongeza sana mkuu wa wilaya ya
Kasulu Kanali Isack Mwakisu, mkurugenzi, madiwani, Chama cha Mapinduzi, wakuu
wa idara, vitengo pamoja na wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu kwa
kazi iliyotukuka, tumeoina miradi katika maeneo mbalimbali tuliyopita na
kuridhika nayo, nami kwa dhati kabisa niseme kuwa halmashauri ya wilaya ya
Kasulu mmeupiga mwingi”, alisema.
Aliongeza pia kuwa, serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi
shupavu wa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan imekuwa ikitoa pesa nyingi kwa ajili ya
kupeleka huduma mbalimbali kwa wananchi hivyo ni jambo la faraja kuona kuwa
pesa hizo mmezisimamia ipasavyo.
Awali baada ya mapokezi yaliyofanyika katika kijiji cha Mvugwe,
mwenge wa uhuru ulianza mbio zake kwa kuzindua majengo ya vyumba viwili vya
madarasa na ofisi ya walimu katika shule ya Msingi ya Kumganza mradi
uliotekelezwa kwa thamani ya shilingi 80,750,000 kupitia ufadhili wa World
Vision.
Miradi mingine iliyotembelewa na mbio za mwenge wa uhuru na
thamani ya miradi hiyo ikiwa kwenye mabano ni pamoja kikundi cha
waendesha bodaboda wa kijiji cha Makere (40,000,000/=), mradi wa bustani ya
kuzalisha miche ya miti katika kijiji cha Kalimangoma (250,000,000/=) na mradi
wa maji safi na salama kwenye kijiji cha Mkesha (253,400,272/=).
AIidha katika eneo la hospitali ya halmashauri ya wilaya ya
Kasulu, kiongozi wa mwenge wa uhuru aliweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa
nyumba nne za watumishi wa hospitali hiyo (460,000,000/=) na katika ujenzi wa
barabara yenye urefu wa nusu kilometa inayotengenezwa kwa kiwango cha rami
kuelekea katika hospitali hiyo (500,000,000/=).
Kabla ya kufika kwenye eneo la mkesha, msafara wa mbio za mwenge
wa uhuru ulizindua klabu ya wapinga rushwa katika shule ya sekondari ya
Rungwampya.
Sanjari na kuzindua, kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya
maendeleo, mwenge wa uhuru umekuwa ukitoa ujumbe wenye kauli mbiu ya kupiga
vita uharibifu wa mazingira, rushwa, matumizi ya dawa za kulevya na kujikinga
na maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI.