Mkutano wa mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoa wa shinyanga waweka maadhimio

       

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza kwenye mkutano Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ambao umefanyika leo Julai 5,2023.

                Na Mapuli Misalaba, Shinyanga                                                               

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
ameyakumbusha mashirika yasiyo ya kiserikali NGO’s yaliyopo mkoani hapa kuhakikisha
yanaendelea kutekeleza miradi inayolenga kulinda na kuheshimu maadili, mila na
desturi za kitanzania kwa ustawi wa Taifa.

Ameyasema hayo leo Jumatano Julai 5,2023 wakati akifungua
mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Shinyanga, kwa lengo
la kutambua mchango wa mashirika hayo pamoja na  kufanya majadiliano
kuhusu ufuasi mzuri wa sheria, kanuni na taratibu katika utekelezaji wa miradi
mbalimbali.

RC Mndeme amesema serikali haitosita kuchukua hatua zaidi za
kisheria kwa shirika lisilo la kiserikali ambalo litabainika kwa makusudi
kujihusisha na miradi ambayo inakiuka maadili, mila na desturi za Kitanzania.

RC Mndeme ametumia nafasi hiyo kuwaelekeza wataalam wa serikali
wa ngazi ya Mkoa na Halmashauri kuhakikisha wanaimarisha uratibu kwenye
mashirika hayo ili kuepuka mrundikano wa mashirika yanayofanya kazi moja katika
eneo moja.

Aidha, akizungumza katika mkutano huo Mwakilishi wa NGO’s
katika Mkoa wa Shinyanga Bwana Venance Muzuka ameiomba serikali ya Mkoa
kuhakikisha inaendelea kuweka mazingira mazuri na rafiki ya utendaji kazi kwa
mashirika hayo, huku akiahidi kuwa mashirika yasiyo ya kiserikali yataendelea
kufanya kazi kwa kufuata sheria, miongozo na taratibu za nchi.

Katika mkutano huo wa
Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanatekeleza majukumu yake Mkoani
Shinyanga pamoja na mambo mengine wameadhimia mambo mbalimbali ikiwemo serikali
kufanya ufuatilia kwa lengo la kutambua uhai wa mashirika yaliyopo ili yaweze
kutoa mchango wa maendeleo Mkoani Shinyanga.

Wameadhimia pia kuwa na vikao
endelevu vya serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa ajili ya kujadili
masuala mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za NGO’s

Pia wameadhimia kuwa, wasajiri
wa NGO’s katika Halmashauri zote Mkoani Shinyanga kuziunganisha NGO’s kubwa na
mashirika madogo ili kujengeana uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Aidha wameadhimia kuwa na
semina za mara kwa mara baina ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Mashirika
yasiyo ya kiserikali ili kuendelea kujengeana uelewa, huku wakiliomba jeshi la
Polisi kitengo cha dawati la jinsia kuweka mazingira rafiki kwa watoto wakati
wa kupokea na kusikiliza kesi mbalimbali ikiwemo kesi za ukatili pamoja na
migogoro ya kifamilia.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza
kwenye mkutano Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ambao umefanyika leo
Julai 5,2023.

Msajili wa mashirika, afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga
Bwana Tedson Ngwale akitoa semina  kwenye
mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga leo
Jumatano Julai 5,2023.

Msajili huyo wa mashirika Bwana Ngwale  ameelezea mambo mbalimbali ikiwemo sera na
sheria zinazosimamia uratibu wa mshirika yasiyo ya kiserikali, taratibu za
usajiri wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali pamoja na maudhui ya kanuni ya
sheria ya NGO’s.

Mwakilishi wa NGO’s katika Mkoa wa Shinyanga Bwana Venance
Muzuka akizungumza kwenye mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali
Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Julai 5,2023.

Afisa elimu na mawasiliano kwa mlipakodi kutoka TRA Mkoa wa
Shinyanga Bi. Semeni Mbeshi akielezea mambo mbalimbali ikiwemo namna ya
mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali kulipa kodi ambapo amesema mashirika
yanawajibu wa kufuata sheria zote za mlipa kodi.

Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Mkoa
wa Shinyanga Bwana Donasian Kessy akizungumza kwenye mkutano huo  wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali
Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Julai 5,2023.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna wa
Polisi Janeth Magomi akiyaomba mashirika kuendelea kushirikiana katika
utekelezaji wa majukumu yao ili kuimarisha usalama.

Mwenyekiti wa kamati ya
amani na maridhiano Mkoa wa shinyanga Shekh Balilusa Khamis akiwasihi
kuzingatia maadili na kushirikiana pamoja katika kutokomeza vitendo vya
ukatili.

Mkutano
wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga ukiendelea leo
Jumatano Julai 5,2023 katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkutano
wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga ukiendelea leo
Jumatano Julai 5,2023 katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkutano
wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga ukiendelea leo
Jumatano Julai 5,2023 katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.



Mwenyekiti wa taasisi ya msaada wa
kisheria Mkoa wa Shinyanga Bwana John Shija
akitoa maoni kwenye mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya
kiserikali ya Mkoa wa Shinyanga  leo
Jumatano Julai 5,2023.

Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya
Leah Josiah
akitoa
maoni kwenye mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Mkoa wa Shinyanga
 leo Jumatano Julai 5,2023.