Dc samizi, kamanda magomi waipongeza smaujata mkoa wa shinyanga


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi
ameipongeza kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania SMAUJATA
Mkoa wa Shinyanga kwa juhudi mbalimbali wanazozifanya katika kupinga ukatili.

Ametoa pongezi hizo leo Julai mosi Mwaka 2023 akiwa
mgeni rasmi kwenye bonanza la kataa uhalifu toa taarifa, ambao limefanyika
katika kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.

DC Samizi amesema SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wamekuwa
mstari wa mbele kupambana na vitendo vya ukatili kwa kuibua pamoja na kutoa
elimu ya ukatili katika sehemu mbalimbali na kwamba amesema serikali inatambua
mchango wao.

Amewasihi viongozi na wanachama wa SMAUJATA Mkoa wa
Shinyanga kuendelea na juhudi hizo za kupambana na ukatili unaoendelea kwenye
familia na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa
Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi naye pamoja na mambo
mengine ameipongeza kampeni ya SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kwa kuendelea
kuisaidia serikali katika hatua za kutokomeza vitendo vya ukatili Mkoani
Shinyanga.

Kamanda Magomi ameahidi kuendelea kushirikiana na
SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga katika utekelezaji wa majukumu ili kuimarisha
usalama hasa kwa wanawake na watoto.

Akizungumza Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga
Bi. Nabila Kisendi kampeni hiyo itaendelea kushirikiana na viongozi wengine
wanaotetea haki na kwamba amesema wataendelea kutoe elimu kwenye jamii ili
iweze kufahamu madhara ya ukatili.

Madam Kisendi ametumia nafasi hiyo kuwaomba wakazi wa
Mkoa wa Shinyanga kuendelea kutoa taarifa za viashiria pamoja na vitendo vya
ukatili ili hatua zaidi ziweze kuchukulia na mamlaka husika.

Kampeni ya SMAUJATA imeanzishwa Mwaka jana na Waziri
wa maendeleo ya jamii jinsia, wanawake na makundi maalum Dkt. Dorothy Gwajima
kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa Bwana Sospeter Bulugu ikiwa
lengo ni kuisaidia serikali kutokomeza ukatili Nchini.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna
msaidizi wa Polisi Janeth Magomi akiipongeza SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga leo
Julai mosi Mwaka 2023 katika bonanza la kata uhalifu toa taarifa.

  

Viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wakishirikia
leo kwenye bonanza la kataa uhalifu toa taarifa kata ya Ndala Manispaa ya
Shinyanga.