Ajali ya basi la kidiaone : polisi arusha wanena mazito, dereva alimvua asakwa

Na Seif Mangwangi,Arusha 

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kimethibitisha kutokea kwa ajali ya gari la kidia one namba T355DTC  leo asubuhi saa12 40 katika eneo la Kikatiti.

Kwa mujibu wa kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Mary Kipesha, ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva aliyekuwa akilipita gari Kingine bila tahadhari na kulazimika kushika breki za ghafla.
ACP Mary amesema breki alizoshika dereva huyo Evod Lyimo zilisababisha gari hilo kuserereka katika eneo hilo lenye utelezi na kuanguka.
Amesema baada ya ajali hiyo dereva alikimbia na hata hivyo jeshi hilo linaendelea kumtafuta ili aweze kufikishwa mahakamani kwa kosa la kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha ajali.
ACP Mary amesema katika ajali hiyo majeruhi ni wawili ambao ni Lyidia Clara na Doreen Kawiche aliyekuwa kondakta wa gari hiyo ambao wote wamelazwa katika hospitali ya Meru wakipatiwa matibabu, na kwamba hakuna mtu yoyote aliyefariki.
Manusura wa ajali hiyo wanasema kuwa gari hiyo ilipata ajali baada ya kujaribu kulifuata gari la kampuni ya BM Coach lililokuwa limelipiga gari la mbele yake na kukutana na gari zingine mbili amba ya Coaster zilizokuwa zikitokea Moshi na hivyo kulazimika kurudi upande wake ghafla huku akishika breki na kuanza kuserereka katika eneo hilo lenye utelezi.