Aliyetaka kutia nia ya ubunge kalenga auwawa …

Wananchi wa Kijiweni Iringa wakiwa amebeba mwili wa marehemu Raymond Mdota aliyeuwawa 
Nguo za marehemu zikiwepo eneo ambalo mauwaji yaliyofanyika 
Askari polisi wakitoka eneo ambalo mwili ulitupwa
Umati wa wananchi ukiwa eneo la tukio bila tahadhari ya virusi vya Corona 
Eneo la klabu cha kijiweni ambako mauwaji yaliyofanyika 
Mwili wa Raymond Mdota ukiwa umetupwa kwenye shamba la mahindi 
……………………………..

Na  Francis  Godwin, Iringa 
MAUAJI ya  kinyama yamefanyika   usiku  wa   ijumaa  kuu Iringa eneo la Kijiweni kata ya Kwakilosa katika Manispaa ya  Iringa  baada ya mhubiri  wa injili na mgombea ubunge mtarajiwa katika  jimbo la Kalenga   Raymond Mdota (46)  kuuwawa  kwa  kuchinjwa shingo yake akiwa katika  huduma ya kuhubiri injili kwenye  klabu  cha Pombe za kienyeji na  mwili  wake kutupwa kwenye mahindi.
Mashuhuda  wa  tukio  hilo  waliozungumza na mwandishi  wa  habari hizi eneo la  tukio  walisema kuwa tukio hilo lilitokea  usiku  wa Ijumaa na  nje ya  chumba  kimoja wapo  cha klabu cha pombe za  kienyeji  kijulikanacho kwa  jila la Kijiweni Klabu .
Walisema kuwa  kabla ya mauwaji hayo Mdota  ambae ni mmoja kati ya walimu  wastaafu alifika  katika  eneo hilo la Klabu  cha Kijiweni  akiwa na radio  yake  kubwa  aliyokuwa akiitokota  huku  ikiwa  inapiga nyimbo  za  dini na kuanza  kuzunguka  chumba kimoja hadi baada ya  kingine  akipiga  muziki  wa dini ya kikristo  kwa  ajili ya kuomboleza  mateso ya  Yesu Kristo  na nyingine za  kufufuka kwa Yesu .
“ Yaania alifika  hapa mida kama  ya saa mbili  usiku akiwa na radio  yake kubwa akipiga nyimbo za dini kwa sauti  kubwa  huku akicheza kwa fuhara na kuwasisitiza  watu kuachana na dhambi na kumgeukia Mungu tulimfurahia  sana hasa  ukizingatia  ilikuwa ni ijumaa kuu ya mateso ya Yesu ila muda  ulipozidi kusogea katika  radio hiyo  hiyo  alianza  kupiga nyimbo za muzidi wa kidunia na kuanza kutangaza siasa kuwa  yeye ni mkazi wa Magumbike na anampango wa  kwenda  kugombea ubunge wa jimbo la kalenga “ alisema mmoja kati ya mashuhuda ambae hakutaka kutaja jina lake.
Alisema  wakati akihubiri  injili alikuwa ameshika rozari  yake  mkononi ila baadae  alipokuwa  akitangaza siasa  alishika skafu yenye  rangi ya bendera ya Taifa  huku  akisisitiza  kuwa  yeye  ndie mbunge  mpya wa kalenga bila kutaja kupitia  chama  gani na wakati   huo  akinywa   pombe aina ya Ulanzi na  kuwanunulia watu pombe  huku akicheza  muziki .
Hata  hivyo  alisema  wakati  muda wa kufunga  klabu hicho ukielekea  kufika wao  waliondoka  na kumwacha yeye na  watu  wachache wakiendelea  kuwepo  kwenye vyumba  vichache  ambavyo vilikuwa havijafungwa  eneo  hilo kabla ya  asubuhi   kuambia tukio  hilo la kuuwawa  kwake .
Johari  Ngeng’ena mjumbe wa  serikali ya  mtaa  wa Kijiweni alisema kuwa mauwaji hayo ni ya kwanza  kwa mwaka huu na kuwa ila  tukio hilo ni la kinyama  zaidi na limewasikitisha  wananchi wa mtaa  huo .
Hata  hivyo  alisema  kuwa  kutokana na tuko  hilo  wanampango wa kukaa nchini  ili  kuangalia uwezekano wa kuanzisha  ulinzi wa jadi  (sungusungu)  pia  kuwataka  wafanyabiara wa  pombe katika eneo hilo kuwa na muda mzuri wa kufunga  na wale  waliolima mahindi mitaani  basi  kupewa  taratibu za  manispaa za  kuacha  kulima mahindi mitaani kwani  mwili wa marehemu huyo umetupwa kwenye mahindi .
Beth Mdeta  ambae ni muuzaji wa chumba ambacho nje mauwaji  hayo yalifanyika  alisema kuwa  kwa upande wake  alifunga  mapema  na kumuacha Mdota  akiwa  kwenye  katika maeneo ya  klabu  hicho na sio ndani ya chumba chake na  kuwa amesikitishwa na kusikia mauwaji hayo yamefayika nje ya  chumba chake .
  Mimi  nilipigiwa  simu asubuhi na majirani zangu  wakinieleza  kuwa nje ya  chumba change kuna mauwaji  yamefanyika maana kuna  damu nyingi na baadhi ya  vitu kama  mabaki ya nguo  yakiwa yametelekezwa  nje  eneo  lenye damu nyingi “
Mwenyekiti wa Klabu  hicho Nicolina Mapunda alisema  kwa  upande wake marehemu  hamfahamu kabisa na hata huo usiku  ambao watu  wanadai walimuona eneo hilo kwa upande wake hakubahatika kukutana nae  zaidi ya  kupigiwa  simu majira ya saa 2 asubuhi  .
Alisema  kuwa  yeye  amekuwa akifanya kazi ndani ya klabu hicho na wafanyabiashara   wenzake  walimwita na kumuonesha  damu  zilizotapakaa eneo hilo japo  alisema  utaratibu wa klabu  hicho kufungwa ni saa 5 usiku  ila siku  hiyo yeye  aliondoka mapema zaidi .
Mwili wa marehemu  huyo ulikutwa  ukiwa  umechinjwa  shingo na kitu chenye ncha kali  huku  viatu  vyake pamoja na radio  yake   vikiwa vimeporwa na wauwaji  hao na mifuko ya suruali  ikiwa  nje kwa maana ya  pesa  alizokuwa nazo  kusachiwa na wauwaji  hao  huku mkononi  akiwa ameshikilia rozari yake.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire  amethibitisha  kutokea kwa  tukio hilo  kuwa  lilitokea majira ya saa10;20 alfajiri na  kuwa  jeshi la polisi linaendelea  kuwasaka  watuhumiwa wa mauwaji hayo