Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Jacob Mwajenga mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa bushushu katika Manispaa ya Shinyanga kwa tuhuma za kumpiga mke wake Debora Rwekama na kisha kumkata mkono wake wa kushoto chanzo cha tukio kinasadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi
kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga George kyando amesema tukio hilo limetokea siku ya Alhamis Septemba 09,majira ya usiku katika mtaa wa Bushushu manispaa ya Shinyanga ambapo mwanaume huyo amedaiwa kumpiga mke wake sehemu mbalimbali za mwili wake na kwamba baada ya kupoteza fahamu alikatwa mkono wake wa kushoto
Kyando amesema kuwa mtuhumiwa baada ya kufanya tukio hilo alimbeba mwanamke huyo mpaka kituo cha polisi wilayani kahama ambapo alitoa taarifa kuwa wamepata ajali wakati wakiwa safarini.
Mwanamke huyo anayejulikana kwa jina la Debora Rwekwama mkazi wa Bushushu katika manispaa ya Shinyanga mwenye umri wa miaka 34 amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama huku hali yake ikitajwa kuwa mbaya.