Askofu sangu kuadhimisha kumbukumbu ya miaka saba ya kuwa askofu

 Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu LIBERATUS SANGU kesho Jumanne tarehe 12.04.2022 ataadhimisha kumbukizi ya miaka saba tangu alipowekwa wakfu na kusimikwa rasmi kuwa askofu wa jimbo la Shinyanga.

Askofu Sangu ambaye ni wa nne kuliongoza jimbo la Shinyanga tangu kuanzishwa kwake mwaka 1956,aliteuliwa na Baba Mtakatifu Francisco kuwa askofu wa Shinyanga Mnamo Februari 2 mwaka 2015 kufuatia kifo cha mtangulizi wake hayati Aloysius Balina.
Askofu Sangu aliwekwa wakfu na kusimikwa rasmi kuwa askofu wa Shinyanga mnamo April 12 mwaka 2015 kupitia Misa maalum iliyoongozwa na askofu mkuu mstaafu wa jimbo kuu la Dar es salaam Mwadhama Polcap Kardinali Pengo.
Misa ya maadhimisho hayo ambayo itakwenda pamoja na kuweka Wakfu Mafuta ya Krisma takatifu pamoja na kubariki mafuta ya Wagonjwa na Wakatukumeni itafanyika katika kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga kunzia saa 4:00 asubuhi na itahudhuiwa na Mapadre,Watawa na Waamini kutoka sehemu mbalimbali za jimbo la Shinyanga.