Bodi ya tmda yavamia mpaka wa namanga, yapokea taarifa ya ukaguzi mpakani

 



Kamati ya Ziara ya
waumbe wa Bodi ya ushauri ya Wizara ya Afya kwa TMDA,wakiwa kwa mkuu
wa mkoa wa Arusha John Mongela, kushoto ni mwenyekiti wa Eric Shitindi,Mkurugenzi Mkuu TMDA,Adam Fimbo,Prof.Appolinary Kamuhabwa na Prof.Said Aboud akifuatiwa katibu Tawala mkoa wa Arusha Athuman Kihamia, kabla ya kuanza safari kuelekea Mpaka wa Namanga kwaajili ya kuangalia utendaji kazi .

      Kamati ya Ziara ya waumbe wa Bodi ya ushauri ya Wizara ya Afya kwa TMDA,mwenyekiti wa Bodi TMDA Eric Shitindi,akifuatiwa na Mkurugenzi  Mkuu wa TMDA Adam Mitangu Fimbo,wa kwanza kushoto ni Prof.Said Aboud mjumbe wa Bodi,pamoja na Prof.Appolinary Kamuhabwa mjumbe wakikagagua nyumba ya Mamlaka hiyo iliyopo mpakani Namanga

Muonekano wa mpaka wa Namanga wilayani Longido Mkoani Arusha

Mkurugenzi Mkuu TMDA Adam Mitangu Fimbo Akiwa katika Forodha ya Namanga

Paul Mali Kamkulu (TRA)Meneja Msaidizi Forodha,Ushirikiano
kati yetu  na taasisi nyingine za serikali ,tunashirikiana vizuri
kuhakikisha kwamba kinachoingia kinakuwa kimepata kibali kutoka TMDA

Mrakibu
Msaidizi Frank Lubilo ,Kaimu Afisa Uhamiaji Mfawidhi akitoa ufafanuzi
kwa Kamati ya Ziara ya waumbe wa Bodi ya ushauri ya Wizara ya Afya kwa
TMDA,walipotembelea Forodha hiyo ya Namanga kuona utendaji kazi
unavyoendelea
 Mkurugenzi mkuu TMDA Akiwa na Kamati ya Ziara ya waumbe wa
Bodi ya ushauri ya Wizara ya Afya kwa TMDA,wakiangalia dawa
zilizofanyiwa ukaguzi tayari kupelekwa maabara hamishika (Minilab Kit) ili kuhakiki ubora wake,forodha ya
Namanga Mkoani Arusha.

Kamati
ya Ziara ya waumbe wa Bodi ya ushauri ya Wizara ya Afya kwa TMDA,wakiwa
katika chumba Cha baridi Cha kuhifadhiwa dawa katika forodha ya Namanga
Mkoani Arusha



Meneja wa Kanda ya Kaskazini TMDA Proches Patrick mwenye (tshirt nyeupe),wa tatu kutoka kushoto (mwenye shati la draft ni Meneja wa huduma za Kisheria TMDA Iskari Fute,wakiwa wamesimama kwenye nyumba ambayo inatumika kwaajili usimamizi wa shughuli za forodha za Namanga

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini (TMDA) katika kuhakikisha kuwa inadhibiti uingizaji wa bidhaa holela nchini ,Kuanzia
julai 2019-januari 2022 jumla ya  magari 3534 yalikaguliwa katika kituo Forodha Namanga ,ili kujiridhisha kuwa magari hayo hayajabeba dawa ambazo hazina vibali vya Mamlaka hiyo.

Aidha katika kuanzia  Julai, 2019 – Januari, 2022 Jumla ya
mizigo 1,508 (dawa 1,216 na vifaa tiba 292) ilikaguliwa kwa ajili ya kuingizwa nchini
na mizigo 605 (dawa 69 na vifaa tiba 536) ilikaguliwa kwa ajili ya kusafirishwa
kwenda nje ya nchi kuanzia Julai, 2019 hadi Januari 2022; baada ya kukidhi matakwa ya kisheria.
 
Akizungumza katika ziara ya wajumbe wa Bodi ya ushauri ya Wizara ya Afya kwa TMDA, katika mpaka wa Namanga Mkoani Arusha, Mwenyekiti wa bodi hiyo 
Eric Shitindi ,alisema kuwa
lengo kuu la ziara hiyo ni kuangalia utendaji kazi unavyoendelea,kujua
changamoto na namna ya kuzitatua.
 
Mara baada ya ziara hiyo Shitindi
alisema kuwa, wameridhishwa na taasisi zote za serikali kwa ushirikiano
mkubwa wanaouonyesha kwa kufanya kazi kwa pamoja,hivyo basi kulingana
na taarifa waliyoipokea kituoni hapo inaonyesha kuwa ,bado wanahitaji
kuongeza idadi ya watumishi, kwani kwa sasa wapo 3 na eneo hilo
linafanya kazi masaa 24 kwa siku 7.

”Kwakweli
ukilinganisha na sehemu nyingine ambazo tumepita tumefurahishwa sana
jinsi ambavyo tunavyotekeleza majukumuyetu Namanga, kwani mpaka huu ni
mkubwa  ambao unaingiza bidhaa nyingi hususani za dawa, wakaguzi tunao
ambao wanafanya kazi yao vizuri ,pia mamlaka hapa zimetupa ofisi nzuri
ya kuhifadhi dawa zile ambazo zinaingia bila utaratibu,lakini bado
kunauhitaji wa watumishi”
  alisema Mwenyekiti Shitindi.

Akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba( TMDA) Adam Mitangu Fimbo,alisema
kazi yao kubwa ni kuhakikisha kuwa bidhaa hizo zinakuwa salama, bora,
fanisi na kulinda afya ya jamii, hivyo katika kutekeleza majukumu wanao
mfumo wa kufanya ukaguzi ,mfumo wa kutoa vibali vya kuingia na kutoka
nje ya nchi, ambapo katika vituo mbalimbali
vya forodha wanakagua bidhaa zote zinazo ingia na kutoka,na kuhakikisha kuwa zinakidhi matakwa ya kisheria
 
”Bidhaa
kwa mfano zinazoingia nchini zinatakiwa ziwe bora salama na fanisi na zisiweze kuleta athari zozote kwa mtumiaji,wakaguzi wanafanya kazi hiyo
masaa 24 kuhakikisha kuwa nchi hii inalindwa hatuingizi bidhaa ambazo
hazifai kwa matumizi ya binadamu kama vile dawa bandia,dawa duni ,ambazo
hazijasajiliwa tunazitafuta kwasababu haziruhusiwi kuingia nchini na
kuwa na kibali maalum cha TMDA”Alisema Fimbo

Fimbo
alisema kuwa katika ziara hiyo ya bodi waliweza kupita katika mipaka ya
Horohoro,Bandari Tanga,Holili,Tarakea mkoani Klimanjaro,na Namanga,
ambapo waliweza
kuzungumza na watendaji katika  forodha hizo na kugundua changamoto kubwa ni  kutokuwepo kwa scanner katika vituo vyote walivyopita.

Hivyo basi kwa kutambua changamoto hiyo TMDA,wameiomba  TRA kuweka SCANNER
ili kusaidia kubaini uwepo wa dawa katika  makontena au magari,ili
iweze kuwa raisi kugundua wale ambao wanaingiza bidhaa za dawa bila
kufuata taratibu,waweze kuzizuia zisiingie nchini na kuweza kuleta
athari kwa binadamu  
 
Amesema
kwa hali ilivyo sasa, dawa bandia nchini ni kama 3% na hiyo inaashiria
kwamba siyo asilimia kubwa kwani wameweka mifumo mizuri inayofanyakazi,
kudhibiti bidhaa kabla hazijaingia ndani ya nchi,hivyo hali siyo mbaya
nchini ukilinganisha na nchi nyingine.
 
Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Kaskazini TMDA Proches Patrick alisema
kuwa,Mamlaka hiyo inachukua sampuli na kufuatilia Usalama wa dawa, vifaa Tiba na
chanjo hususani chanjo za UVIKO 19, pamoja na kukagua na kusajili
viwanda na majengo ya kuuzia bidhaa zinazoodhibitiwa na Mamlaka hiyo.


Proches alisema maabara iliyopo Namanga  imeshafanya uchunguzi wa sampuli 173 za dawa za
binadamu
zilizoingizwa kutoka nje ya nchi, na sampuli zote zilifaulu
na kuruhusiwa kuingizwa
nchini,hivyo TMDA inaendelea  na zoezi la kuondoa kwenye soko bidhaa
zisizofaa kwa matumizi,kutoa
Elimu kwa umma juu ya matumizi sahihi ya Dawa vifaa Tiba,vitendanishi
na vupukusi.

Akielezea changamoto zilizopo ,alisema  baadhi ya wafanyabiashara huingiza 
bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi pasipo kuzingatia matakwa ya Sheria
ya Dawa na Vifaa Tiba, Sura ya 219 na kutoa visingizio kuwa mizigo hiyo
ililetwa Tanzania kimakosa.

Mafanikio kuwa ni pamoja na kupata Ofisi rasmi ya
TMDA pamoja na
vitendea kazi na hivyo kuboresha utendaji kazi katika mpaka
huo, chumba
kingine maalum kinachotumika kwa ajili ya uchunguzi wa
sampuli za dawa za binadamu
kwa kutumia maabara hamishika (Minilab. Kuanzia Julai, 2019
hadi Januari, 2022

 Paul Mali Kamkulu
(TRA)Idara ya Forodha na Ushuru,alisema kuwa Ushirikiano kati wao  na
taasisi
nyingine za serikali ,wanashirikiana vizuri kuhakikisha kwamba
kinachoingia kinakuwa kimepata kibali kutoka TMDA,na kuahakikisha kuwa
sheria zote katika maeneo yao ya utendaji kazi zinafuatwa kama
inavyohitajika

Ameiomba serikali kuangalia changamoto ya maeneo ya makazi yamekuwa tatizo kwa wafanyakazi tofautitofauti waliopo mpakani,kwani
wamejikuta wakipanga nyumba kwenye maeneo ya wateja wao wakati mwingine
haohao ndio wanakuwa wanaleta bidhaa ambazo siyo sahihi na
zisizohitajika.

Kamkulu amesema kuwa pamoja na hayo wanaendelea kupambana wanahakikisha vitu vyote vinavyoingia vinakuwa katika utaratibu,ila makusanyo kama TRA  waliyoatiwa ,ambapo amesema kuwa hadi sasa wapo 100%

Tunatakiwa kukusanya bil.tano ila hadi sasa tumeshakusanya  tumeshakusanya bil.sita  kwa maana hiyo tutakapofika mwisho wa mwezi tutakusanya zaidi ya hiyo.

 Kwa upande wake  Mfawidhi kutoka TMDA forodha ya Namanga Vedasto Uiso alisema kuwa, kazi kubwa inayofanyika katika kituo hicho ni pamoja na  ukaguzi wa
dawa, vifaa tiba na vitendanishi
pamoja na  kupokea maoni yao kwa kutumia fomu ya Customer Exit questionnaire. 

Pia, kituo hicho hufanya uchunguzi wa sampuli za dawa za
binadamu,kwa kutumia
maabara hamishika (Minilab Kit) ili kuhakiki ubora wake,kwani forodha hiyo ni moja ya vituo ambavyo vinafanya
kaguzi za mizigo kwa
upande mmoja tu wa nchi (One Stop Border Post – OSBP) ambapo
mizigo
inakaguliwa kwa pamoja na wakaguzi wa nchi zote mbili