Na Magesa Magesa,Arusha
SERIKALI Imeitaka benki kuu [BOT] kuhakikisha kuwa inasimamia kanuni ,taratibu na sheria katika kuhakikisha benki zote nchini zinafanya kazi zao kwa kuzingatia weledi katika kuwahudumia wananchi
Waziri wa Fedha na mipango,Dkt Mwigulu Nchemba,aliyasea hayo jana alipokuwa akizindua tawi jipya la benki ya Mwanga Hakika benki na kuitaka benki hiyo kujiendesha kwa kutoa huduma nzuri na bora kwa wateja wake .
Amewashauri wateja waliokopa katika taasisi za fedha kuhakikisha wanarejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kuwezesha wengine nao kukopa kwa kuwa benki zimesaidia ukuaji wa pato la taifa kwa mtu mmoja mmoja
‘’ Watu wanaomba fedha kwenye taasisi za kifedha lakini hawana malengo nayo ,ninawaonya maafisa wote wa benki kuhakikisha kuwa kila mkopaji awe na lengo linaloeleweka ili aweze kurejesha kwa wakati “alisisitiza Dkt Nchemba
Waziri ,huyo aliwataka wananchi kuwa na nidhamu ya mikopo kwani watu wengi wamekuwa wakichukua mikopo hawajui wanaifanyia nini kwa kuwa hawajajiandaa nashughuli watakayoifanyia mikopo hiyo.
Nae Mwenyekiti wa bodi ya Mwanga hakika benki, Ridhiwani Mringo,amesema kuwa benki hiyo imejipambanua katika kuwahudumia wateja wengi zaidi ambapo itatoa faida kwa wenye hisa na wateja wengine wa benki hiyo ,.
Mringo, amesema kuwa benki zimesaidia ukuaji wa uchumi na hivyo kuongeza pato la mtu mmoja mmoja.
Nae Mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo ,Jagjit Singh , amesema benki hiyo ilianza mwaka 1998 ikiwa ni benki ya kijamii na mwaka 2020 ilikuwa ni benki ya Microphinance na kuanzia mwaka 2022 mpaka sasa ni benki ya biashara.
Mkurugenzi huyo alisema kwamba lengo ni kuifanya iwe ya kimataifa zaidi kutoka nchini hadi itoe huduma zake ukanda wa Afrika mashariki lengo ni kuhudumia watu wengi zaidi na kwamba benki hiyo inatoa riba ya asilimia 12% kwa atake weka akiba .