Breaking news rais samia atengua uteuzi wa katibu mkuu ikulu

*Ni Diwani Athumani, aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa

Na Mwandishi Wetu,
Taarifa iliyotolewa Leo Januari5,2023, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Ikulu Diwani Athumani aliyemteua siku mbili zilizopita, Oktoba 3,2023.
Diwani Athumani aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu,  huku  watu wengi wakibakiwa na maswali mengi yasiyokuwa na majibu kutokana na nafasi nyeti aliyokuwa nayo ya Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa.
Aidha Rais Samia amemteua Mululi Majula Mahendeka kuwa Katibu Mkuu Ikulu akichukua nafasi ya Diwani Athumani.
Hata hivyo pamoja na uteuzi huo, Taarifa ya Mkurugenzi wa Ikulu Zuhura Yunus haijasema Diwani Athumani amepangiwa kazi gani nyingine.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *