Breaking news: watu 62 wamekufa,70 kujeruhiwa baada ya lori la mafuta kuwaka moto moro

Na Mwandishi Wetu, APC BLOG, MOROGORO
WATU 62 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine 70 kulazwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro baada ya lori la mafuta kupinduka na kulipuka katika ajali iliyotokea eneo la Msamvu Morogoro.

Inadaiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mmoja wa wakazi katika eneo hilo kutaka kuiba betri ya gari hilo la mafuta ndipo lilipolipuka na kuanza kuunguza watu waliokuwa wakichota mafuta yaliyomwagwa na gari hilo sanjari na watu waliokuwa jirani wakiendelea na biashara zao. Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro