Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akimkabidhi Nahodha wa timu ya Simu banking kombe mara baada ya kushika nafasi ya Kwanza katika fainali za CRDB super cup
|
Na Woinde shizza , Arusha
Timu ya mpira wa Pete ya Tanzanite queen pamoja na timu ya mpira wa miguu ya simu banking imeweza kuibuka kidedea na kunyakua kitita ela pamoja na makombe katika mashindano ya CRDB super cup.
Akizungumzia mashindano hayo mkurugenzi wa rasilimali watu kutoka benki ya CRDB Siaopharo Kishimbo alisema kuwa mashindano hayo yalianza kutimua vumbi mapema mwezi September mwaka huu ambapo mashindano hayo yalishirikisha timu kutoka katika matawi yote ya benki hiyo Tanzania nzima.
“Tulishirikisha timu zote katika matawi baada ya apo zikachujwa hadi zikabaki timu za kanda na makao makuu ambapo jumla zilikuwa 16 Kwa mpira wa miguu pamoja na timu nane za mpira wa Pete”alisema Kishimbo
Alitaja timu zilizoibuka kidedea Kwa upande wa mpira wa miguu timu ya Simu banking ilifanikiwa kushika nafasi ya Kwanza ambapo ilifanikiwa kuondoka na kitita cha shilingi milioni tano ,medali pamoja na kombe huku nafasi ya pili ikishikiliwa na timu ya makao makuu ya crdb(HQ)ambapo iliondoka na kitita cha shilingi milioni tatu ,kombe na medali huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na timu ya Nia Fc ambayo ilifanikiwa kuondoka na kitita cha shilingi milioni moja.
Kwa upande wa mpira wa Pete timu ya Tanzanite queen iliibuka kidedea na kufanikiwa kuondoka na kitita cha shilingi milioni tatu ,kombe na medali huku nafasi ya pili ikishikiliwa na timu ya ulipo tupo ambayo iliondoka na kitita cha shilingi milioni mbili ,medali na kombe huku nafasi ya tatu ikishikiliwa hodari Queen ambayo ilifanikiwa kuondoka na kitita cha shilingi milioni moja kombe pamoja na medali.
Akizungumzia mashindano hayo mara baada ya kukabidhi makombe
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema kuwa nia yakuandaa mashindano hayo ni kuwaletea pamoja wafanyakazi wa benki hiyo na kibadilishana uzoefu na ujuzi pamoja na kuhamasishana kufanya mazoezi
Alisema kuwa hii ni mara ya Kwanza mashindano hayo kufanyika na hayataishia hapa bali yatakuwa yanafanyika Kila mwaka .
Aliwasihi wafanyakazi wa benki hiyo kuendelea kufanya michezo na mazoezi kwani michezo inasaidia kujenga ushirikiano mzuri pamoja na kuendelea kutengeneza afya .
Alisema kuwa zipo changamoto mbalimbali ambazo wamekutana nazo katika mashindano haya ikiwemo ya uhaba wa viwanja vya kufanyika mazoezi Kwa timu zao na kubainisha kuwa katika michezo ijayo wataangalia namna ya kuzitatua mapema.
Timu ya mpira wa Pete ya Tanzanite queen wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi kombe fedha taslimu kiasi Cha shilingi milioni tatu
|