Dc asia aruhusu wananchi kuandamana kwenda shamba kulima

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Mkoani Iringa Asia
MKUU  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdallah amewataa  wananchi  wa  wilaya  hiyo kujikita zaidi katika maandamano ya  shambani na katika shughuli za  kimaendeleo badala ya  kuwasikiliza waliokuwa wagombea wa nafasi mbali mbali  wanaowaza kuvuruga  amani kwa kutamani maandamano yasiyo na  tija ya  kiuchumi .Mwandishi  Francis  Godwin  anaripoti kutoka  Iringa


Akizungumza jana na kituo cha matukio daima Tv mkuu   huyo wa wilaya  alisema  kuwa wananchi  wanapaswa  kutambua  kuwa  muda wa kampeni kwa  ajili ya  kupata  viongozi  watakaowatumikia kwa  kipindi cha miaka mitano umekwisha pita na  sasa  ni wakati wa  wananchi pamoja na  viongozi hao kufanya kazi .

Hivyo  alisema  itakuwa  si  sawa kwa  mwananchi wa Kilolo  kuacha  kufanya  shughuli za  kimaendeleo na  kushughulishwa na maandamano  yasiyo na  tija katika ustawi wa maisha yao .

”  Tunahitaji  kuona  wanasiasa  sasa  wanashiriki katika  ujenzi wa Taifa  kwa  kuhamasisha  wananchi  kufanya  shughuli za kimaendeleo  kuliko  kuhamasisha  wananchi kwenda  barabarani  kuandamana”
Mkuu   huyo wa  wilaya  aliwataka  vijana  wilaya ya  kilolo  kuwapuuza  wale  wote  ambao  wanatamani  kuona  amani ya  nchi hii inavurugwa  kwa  kutamani maandamano na  vurugu  badala yake  anatamani  kuona  kila  kijana  anajishughulisha katika kazi za uzalishaji mali .

Asia  alisema katika  wilaya ya Kilolo uchaguzi  umefanyika katika hali ya amani na utulivu mkubwa na kuwapongeza  wananchi kwa  kutimiza wajibu  wao wa  kikatiba kwa amani na utulivu pia  kuwapongeza  wale  ambao  wamechaguliwa  kuwa viongozi  akiwemo Rais Dkt  John  Magufuli ,mbunge wa  kilolo Justin Nyamoga na madiwani  wote  waliochaguliwa .

Aidha  aliwataka  wazazi wilayani humo  kuendelea na maandalizi ya kuwapeleka  watoto  wao shule  hapo mwakani .

Kwani  alisema  ni   jukumu la kila mzazi ama mlezi kuhakikisha  mtoto wake anapata  elimu na anasimamiwa  vema  ili  kupata elimu  hiyo mwanzo hadi mwisho  bila  kukatishwa masomo ama mzazi  kumgeuza mtoto  huyo kuwa ni  sehemu ya watafutaji wa fedha  za familia .

Alisema  kwa  wale  watoto  waliohitimu  elimu ya msingi  wazazi  kuendelea kuwalea  kwa   kuwalinda watoto hao  ili  wasirubuniwe na mtu yeyote  kwenda  mijini kufanya kazi za ndani ama kupewa mimba kwa  wale wa kike.

”   Serikali hii  chini ya  Rais  Dkt  John  Magufuli  imeendelea  kuboresha  mazingira bora ya  elimu  kwa  kuondoa changamoto  mbali  mbali katika  elimu hata  kuamua  kufuta  ada kwa  elimu  msingi ” alisema
Hivyo  alisema  jukumu la  mzazi na mlezi ni kusimamia  watoto  kwenda shule  na  kuwalinda na vikwazo ambazo  vinaweza  kuwavurugia masomo yao  na   sio  wasimamizi hao wa  mtoto  kuwa  chanzo cha  kuwaharibia maisha  watoto hao  kutofikia ndoto  za  serikali za  elimu  bora.

Asia  alisema   serikali haitaacha  kuwachukulia  hatua  wazazi ama  walezi ambao watabainika   kuwakwamisha  watoto   wanaopaswa  kwenda   sekondari ama  kupata  elimu .
Kuhusu