Dna ya kilimo yawa suluhisho la wakulima

 

div class=”separator” style=”clear: both; text-align: center;”>

 Dkt. Joseph Ndunguru akitoa semina katika moja ya ukumbi uliopo katika Chuo Cha Nelson Mandela kilichopo Jijini Arusha 
Baadhi ya Washiriki wa semina hiyo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela  kilichopo jijini Arusha wakifuatilia kile kinachoendelea katika mafunzo hayo.

 Dkt. Joseph Ndunguru akitoa semina katika katika Chuo cha Nelson Mandela kilichopo Jijini Arusha .


DNA YA KILIMO YAWA SULUHISHO LA WAKULIMA

Na.Vero Ignatus,Arusha

Kituo cha Utafiti wa Mazao ya Kilimo cha TARI Seliani hapa jijini Arusha kimeanza mpango mkakati wa kutoa semina ya kuwajengea uwezo wanasayansi chipukizi  waliopo vyuoni kuhusu Teknolojia ya Upimaji wa DNA ili wawe kuwa mabalozi wa kuwaelimisha Watanzania kuitumia kwa ajili ya kuwa na uthibiti endelevu wa visumbufu vya mazao.

Akizungumza  baada ya kutoa semina kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela  kilichopo jijini Arusha Mkurugenzi wa kituo hicho Dkt. Joseph Ndunguru amesema lengo kuendelea kutoa elimu zaidi kwa  wanasayansi chipukizi ili  wawe wakufunzi kwa wengine ili kuleta tija katika shughuli za kilimo na ufugaji kukuza uchumi wa mkulima na taifa kwa ujumla.

Dkt. Ndunguru amesema tayari Teknolojia hiyo imeanza kutumika hapa nchini Tanzania na imekuwa msaada mkubwa kupata suluhisho la changamoto zinazokabili sekta ya kilimo na ufugaji pamoja na maeneo mengine ili kusaidia kukuza uchumi na kuzalisha kwa tija kuelekea Tanzania ya viwanda 2025.

Dokta Ndunguru ameongeza kuwa nchi ya Jumuiya wanachama zipo katika mkakati wa kubadilishana mbegu mbalimbali za kilimo; hivyo tekonolijia hiyo itawezesha kusaidia kutambua uhalali na ubora wa mbegu kutoka nchi husika katika maeneo ya mipakani  pamoja na kuboresha mahusiano ya kibishara baina ya nchi hizo.

Aidha amesema kuwa teknolojia hiyo pia itakuwa msaada mkubwa sana katika mazao ya bahari kuweza kutambua samaki hata akisafirishwa  nchi nyingine ili kuendelea kulinda rasilimali za nchi ya Tanzania na kulinda viwanda vya ndani.

Dkt.Ndunguru amesema kuwa ipo haja maafisa ugani kuweza kutumia teknolojia hizo kwa vitendo ili kuweza kuakisi na kutatua matatizo yanayowakabili wakulima na wafugali ili kuweza kutatua changamoto za wakulima na wafugaji ambazo kwa sasa wanakabiliana nazo ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi,pembejeo feki hasa msimu wakilimo  ili kuleta tija na pia kunusuru kundi hilo na hasara wanazipata katika msimu wa kilimo na mavuno.

Kwa upande wake Mhadhiri katika taasisi hiyo ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Dkt Isakwisa Ngondiya amesema ipo haja kwa wafanyakazi katika taasisi za Sayansi na Teknolojia kufanya tafiti ambazo zitaleta tija na kuharakisha maendeleo ya nchi yetu Na kufikia lengo la kuwa na Tanzania ya viwanda.

Kwa upande wao wanataaluma Scolastika na Lyimo kutoka chuoni hapo wamesema kuwa   elimu ya Teknolojia  ya Upimaji DNA imekuja muda muafaka  na kuweza kupata suluhisho la kudumu hususani kuonganisha tafiti za masuala ya kisayansi na teknolojia katika kukuza uchumi na maendeleo jamii kwani ikitumika vizuri italeta tija kwa wakulima na  wafugaji taifa kwa ujumla.

Hata hivyo wameiomba serikali kushirikiana na taasisi na vyuo kuendelea kutoa elimu ya teknolojia hiyo kwa kuweza kuendelea kutunza rasilimali zilizoko na kupata suluhisho la kudumu la visumbufu vya mimea na maeneo mbalimbali ili kuweza kunusuru kundi hilo kwa maslahi mapana ya taifa la Tanzani.

MWISHO.