Elimu ya awali,mkombozi wa mtoto anayeanza shule

 Joyce   Joliga,Songea

Siku zote nyumba huanza na msingi, na hata katika safari ya elimu huanza  na shule ya chekechea au awali, Elimu ni nguzo muhimu katika jamii na ndio ufunguo wa maisha.

Ili kuleta usawa katika jamii, juhudi nyingi zimeongezwa kasi ili bidhaa hiyo iwafikie watoto na vijana wa jinsia zote mbili kwa mujibu wa ripoti ya karibuni iliyotolewa na mashirika ya Umoja wa Mataifa japo imetoa angalizo kwamba maeneo ya vijijini bado yamesalia nyuma hata baada ya harakati kuimarishwa. 

Ripoti hiyo ya pamoja ya shirika la umoja wa mataifa la elimu na utamaduni, UNESCO na lile la kuhudumia watoto UNICEF na wadau iliyotokana na utafiti imebaini kuwa idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika ilipungua kwa milioni 7.7 katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. 

Elimu kwa maana pana ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika dhana ya kiufundi, elimu ni njia ambayo hutumiwa makusudi na jamii kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine.

Kwa Manispaa ya songea uandishikaji wa  awali uevuka lengo ambapo hadi sasa uandikishaji ni asilimia 106 na tayari  Manispaa  imeshavuka lengo 102, ingawa changamoto hazijakosekana kwa wazazi au walezi kuchelewa kuwaandikisha wanafunzi wa awali kwa mfano  Watoto kutumiwa na wazazi wao kwaajili ya kufanya biashara au wazazi kuhama makazi na Watoto wao

Balozi wa Watoto mkoa wa Ruvuma na mwandishi wa Habari Joyce Joliga anasema kuwa kuna umuhimu kwa wazazi na walezi kuwaandikisha Watoto wao darasa la awali kwakuwa elimu ya awali ndio msingi wa mtoto.

Dominica Nungu ni  mwalimu wa darasa la awali shule ya miembeni amesema kuwa mbinu shirikishi imekuwa ikiwasaidia wanafunzi ili kuona kama mwanafunzi ameelewa, ingawa changamoto iliyopo uchache wa walimu wa darasa la awali kwakuwa darasa lake lina wanafunzi 171.

Kutokana na changamoto ya uchache wa madarasa,madawati na walimu je serikali imejipanga vipi kuhakikisha wanatatua changamoto hizi?  Afisa Elimu   Manispaa ya Songea Frank Sichalwe anasema ni kweli bado kuna chagamoto mbali mbali zozinawakabili kwenye sekta ya elimu ikiwemo upungufu wa walimu, hasa walimu  wa awali lakini wanajitahidi kuhakikisha  wanafundisha kwa bidii  ili watoto wapate elimu bora na siyo bora elimu ili waweze kuingia darasa la  kwanza  wakiwa wanajua kusoma,kuhesabu  na kandika.

Aidha,ametoa  ushauri kwa Wazazi kupeleka watoto wao kuanza masomo ya awali ili kuweza kupata elimu ya awali