Ewura kaskazini yawasihi wauzaji wa mafuta kutoyaficha

Na Mwandishi Wetu,Arusha

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kanda ya kaskazini imewataka wafanyabiashara wa mafuta kuhakikisha kuwa wanafuata taratibu za biashara hiyo na kuachana na tabia ya kuficha mafuta kwani kwa kufanya hivyo wana kiuka taratibu.

Pia mamlaka hiyo imewataka wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanakuwa na  mikataba ambayo itaweza kuwasaidia kupata mafuta kwa uraisi.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Ewura Kanda ya kaskazini, Mhandisi Lorivini Lon’gidu alipokuwa akizungumza na wamiliki wa vituo vya mafuta Kanda ya kaskazini jijini Arusha juzi.

Lorivini alisema ni muhimu kwa wafanyabiashara wa mafuta kuhakikisha kuwa wanakuwa waaminifu ikiwa ni pamoja na kutoficha mafuta hali ambayk wakati mwingine husababisha madhara kwa watumiaji wa mafuta

“Ni muimu sana kwa wafanyabiashara wa mafuta kuhakikisha kuwa sasa kila mmoja anafuta kanuni n sheria na pia tutambue kuwa mfanyabiashara mmojawapo anapokiuka sheria anasababisha shida kubwa na tusikubali hilo kabisa”aliongeza

Mbali na hayo alisema mamlaka hiyo inawataka wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanauza mafuta bila kuwa na upendeleo wa aina yoyote.

“Huduma ya mafuta inatakiwa ifike kila maali kusiwepo na changamoto ya aina yoyote ile kwa kuwa mpaka sasa mafuta hasa kwa kanda ya kaskazini yapo tena ya kutosha”alisema

Alimalizia kwa kusema kuwa mamlaka hiyo sasa itaendelea kukutana na wafanyabiashara mara kwa mara ikiwa ni kwa ajili ya kukumbushana umuhimu wa kufuata sheria na kanuni za uuzaji wa mafuta.