Washiriki katika kikao cha ushauri Mkoa (RCC) Mbele Upande wa Kulia ni Mkuu wa Wilaya Arusha Felician Mtahengerwa |
Egidia vedasto
Arusha
Wakurugenzi na Wakuu wa wilaya wametakiwa kusimamia ukusanyaji mapato kwa nafasi zao ipasavyo ili kufikia malengo yaliyowekwa ifikapo mwisho wa mwaka huu.
Akizungumza katika kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa ( RCC )kujadili makadirio ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika jijini Arusha Mkuu wa wilaya Karatu, Dadi Kolimba, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Arusha John Mongela amesema mapato katika halmashauri zote za mkoa wa arusha yameongezeka.
Aidha ametoa maelekezo juu ya hoja iliyoibuliwa katika halmashauri ya Arusha kuwepo na baadhi ya watumishi wanaoshirikiana na wafanyabiashara kuhujumu uchumi kwa kuwapunguzia makadirio ya mapato wanayotakiwa kutoa kwa lengo la kujinufaisha wenyewe hatua ambayo inadumaza jitihada za ukusanyaji na kupelekea kutofikia malengo.
Kolimba amemtaka Mkuu wa wilaya ya arusha Felician Mtahengerwa kuchukua hatua za haraka kwa watumishi wote wanaokusanya mapato wanaohujihusisha na vitendo hivyo kwani ni kurudisha nyuma maendeleo ya halmashauri na taifa kwa ujumla.
Hatahivyo, Mkoa wa Arusha umepitisha shilingi bilioni 406.081 katika bajeti ya mwaka 2024/2025 ambapo kila halmashauri itakusanya bilioni 81 tofauti na bajeti ya mwaka 2023/2024 ambayo kila halmashauri ilitakiwa kukusanya bilioni 75.
Sambamba na hayo kolimba ameagiza halmashauri ya wilaya Ngorongoro na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kukutana na kujadili suala la mapato yanayopatikana kutokana na hifadhi, ili kupata ufafanuzi juu ya mapato yatakayokwenda kwenye halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro.
“Ikishindikana kupatikana majibu ya kueleweka basi suala hilo itabidi lipelekwe kwa Mkuu wa Mkoa John Mongela ili kupata muafaka utakaoweka mambo sawa katika utendaji, kama nilivyoagiza kwamba ufanyike uchunguzi kwanini Kamishna huyo hakufika katika kikao hiki kama hakuna sababu za msingi basi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake” Amesema Kolimba.
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Mussa Missile alisoma ajenda za kikao, Kulia ni Mkuu wa wilaya Karatu Dadi Kolimba akipitia mambo mhimu katika kikao hicho cha (RCC) Jijini Arusha |
Mjadala huo umekuja baada ya watumishi wa halmasahauri ya wilaya ya Ngorongoro kumlalamikia Kamishna Mhifadhi wa hifadhi ya Ngorongoro ambaye hakuhudhuria kikao hicho.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Arusha Felician Mtahengerwa amesema kwamba utafiti ufanyike katika halmashauri zote kubaini vyanzo vya mapato vilivyopo ili viwiane na mapato yanayokusanywa.
Akizungumza katika kikao hicho ameeleza kwamba halmashauri ya wilaya ya Arusha kwa robo ya mwaka mwaka wa fedha 2023/2024 imekusanya bilioni 27 sawa na asilimia 56.
“Kwa mfano wilaya ya Arusha inazidiwa na wilaya ya Karatu kwa wingi wa hoteli ambazo zinaingiza kipato kikubwa lakini bajeti waliyojiwekea wao ni ndogo, pia Wilaya ya Monduli imeonekana kuwa juu katika ukusanyaji mapato ya zaidi ya bilioni moja sawa na asilimia 74, unaweza kuona ni jinsi gani halmashauri zingine hazifanyi utafiti kuweka uwiano sawa kati ya vyanzo halisi na mapato yake” amefafanua Mtahengerwa.
Mkuu wa wilaya Longido Marco Ng’umbi akielezea namna wamejipanga kuanzisha vyanzo vipya vya mapato |
“Kila mwanzo wa wiki tumeweka utaratibu wa kukaa na kujadili mapato yote yanayopatikana kila wiki na kuhakikisha hayakai mikononi mwa wakusanyaji kwa siku mbili kabla ya kupelekwa benki, hii njia imesaidia sana kwani pesa nyingi zilikuwa zinaliwa kwa sababu ya kukaa kwa wakusanyaji muda mrefu kabla ya kupelekwa panapohusika” amesema Ng’umbi.
Ng’umbi ameeleza mipango waliyojiwekea kuongeza mapato badala ya kutegemea sekta ya mifugo ambayo ni tegemeo kwa asilimia 99, na kuweka wazi mikakati ya kuanzisha stendi ya kisasa, kujenga parking ya maroli ya kubeba zaidi ya maroli 500 katika eneo la Olendeka, Namanga na kujenga soko la kisasa.
Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Kanali Wilson Sakulo amesema ukusanyaji wa mapato katika wilaya yake umeongezeka kutoka laki nane hadi milioni tatu kwa wiki.
“Naamini kwa mabadiliko haya ya ukusanyaji mapato ni makubwa kiasi kwamba yatapandisha kiwango na kufa
Mkuu wa wilaya Ngorongoro Kanali Wilson Sakulo akifafanua kuongezeka kwa mapato katika wilaya yake leo Jijini Arusha |