Jamii yaaswa kulinda haki za watoto

 Na Frankius Cleophace Tarime.

Jamii imehaswa kulinda na kutetea haki za watoto ili waweze kupata malezi na makuzi bora kwa lengo la kupata ustawi.

 Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa Dawati la Jinsia mkoa wa polisi Tarime Rorya SP: Fatma Mbwana katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga Ukatili wa kijinsia.

 Maadhimisho hayo yamezinduliwa katika kata ya Nyamwaga wilayani Tarime mkoani Mara  ambapo wanafunzi, wazazi na mashirika pamoja na taasisi mbalimbali zimeweza kushiriki katika uzinduzi huo nia ni kuendelea kupaza sauti ili jamii iweze kuondokana na vitendo vya ukatili.

 Fatma alisema kuwa kumekuwepo na matukio ya kutelekeza watoto wachanga jambo ambalo ni la ukatili kwani watoto hao wana haki za kuishi hivyo ameitaka jamii kuondokana na ukatili huo.

“Mzazi kweli unabeba ujauzito miezi tisa inafika hatua unaenda kutupa mtoto jambo ambalo hata mwenyzi Mungu hapendi sasa tutumie siku kumi na sita hizi kuendeea kutoa elimu na sisi jeshi la polisi Tarime Rorya tunaendelea kutoa elimu kwa jamii ili iweze kubadilika” alisema Fatma.

 Licha ya kutelekeza kwa watoto Fatma liongeza kuwa kumekuwepo na matukio ya kuchoma moto watoto na kuwafanyia ukatili mwingine jambo ambalo serikali haikubaliani nalo hivyo jamii ibadilike ili kulinda haki za watoto hao.

Nao baadhi ya washiriki katika  ufunguzi huo wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatilii wameiomba serikali kuendelea kuchukua hatua kali kwa wale wote wanatenda ukatili kwa watoto.

Ikumbukwe malezi ya watoto yanajumuisha watu wawIli Baba na Mmama hivyo sasa ni vyema kila mtu awezer kutimiza wajibu wake ili watoto wakue katika misingi bora