Jatu yazindua program ya kumbana na tatizo la ajira

Kutokana na changamoto ya ukosefu wa ajira nchini Tanzania kwa vijana wengi hasa wanapohitimu mavyuoni, kampuni inayojihusisha na uwekezaji wa kilimo JATU Plc imezindua program Maalimu (Unitalk) kwa lengo la kupambana na tatizo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Mohamed Simbano wakati akimtambulisha balozi mpya wa kampuni hiyo Quen Elizabeth amesema kuwa program hiyo itakua mkombozi kwa vijana wengi.

Amesema kuwa, kampuni hiyo imekua ikifanya kazi kwa kushirikiana na Serikali katika kupambana na tatizo la ajira kwa kuanzisha mipango na mikakati mizuri kwa wananchi ili ifikapo 2025 Tanzania kuwe na viwanda vingi zaidi ambavyo vitaweza kupunguza tatizo la ajira.

Kwa upande wake, Balozi wa Kampuni hiyo, aliekua  Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth amesema asilimia kubwa ya vijana mavyuoni hawana uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya Kilimo na masoko hivyo kuanzishwa kwa program hiyo itaweza kutoa mabadiliko makubwa kwa vijana .

“Vijana wengi wanapokua mavyuoni hua na ndoto za kuajira mara wapomaliza masomo,  wanaposhindwa kuajiriwa hupoteza ndoto zao, hivyo kupitia Unitalk(mazumgumzo ya wanafunzi wa vyuo vikuu) tutaweza kuwafikia vijana wengi zaidi ili kuwaelimisha”amesema Quen Elizabeth.

Ameongeza kuwa, program hiyo itaanza kwa mikoa 10 huku wakianzia na mkoa wa  Dar es Salaam lengo lilikiwa ni kutoa elimu kuhusu kilimo masoko na uwekezaji ili watakapo maliza chuo waweze kujiajiri wenyewe badala ya kufikiria kuajiriwa.

Naye Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Marry Chulle, amesema katika kukuza soko la ajira wameanzisha wanaprogram ya ‘Kula Ulipwe’ inayomwezesha mteja kupata asilimia 30 kila anapofanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo.

“Kupitia kampeni hii itawawezesha vijana kuweza kujiekea akiba hata wanapofanya manunuzi ya kawaida kwani wanapata faida kuanzia asilimia 30, unapata faida mara mbili chakula halafu unalipwa, niwaombe vijana kama bado hamjaingia kwenye akaunti yetu karibuni”amesema Chulle.