Baadhi ya magari yaliyokutwa na makosa mbalimbali ambapo yaling’olewa namba hadi pale watakaporekebisha makosa hayo.Picha na Vero Ignatus. |
Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Arusha Solomoni Mwangamilo akizungumza na baadhi ya madereva wa magari ya kubeba wanafunzi kwa shule binafsi Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus. |
Baadhi ya magari yaliyokutwa na makosa mbalimbali yakiwa yameng’olewa namba hadimpale wamiliki wao watakaporekebisha makosa hayo .Picha na Vero Ignatus. |
Na.Vero
Ignatus,Arusha
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani kimeendesha zoezi mahususi kwa ukaguzi wa
vyombo vya moto wakiwa wamejikita kwenye magari yanayobeba wanafunzi,ambapo
magari zaidi ya 163 yamekaguliwa huku magari 17 yakiondolewa namba zake za
usajili kutokana na kukutwa na makosa mbalimbali.
Mrakibu wa Polisi
na Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Arusha Solomoni Mwangamilo
akizungumza na Michuzi Blog, amewataka
wamiliki wote wenye magari ya shule kuyapeleke vituo vilivyoainishwa kwaajili
ya ukaguzi kwani msako utaanza siku ya jumatatu kwa magari yote ambayo hayana
hati ya ukaguzi ambapo hatua stahiki itachukuliwa
Mwangamilo amesema kuwa Jeshi la polisi mbali
na kuangalia usalama wa rai na mali zao pia wamejikita kwenye ‘’Usalama wa
mtoto’’hivyo hawataruhusu kuona magari ambayo hayajakaguliwa kuwa
barabarani,kwani baadhi yamefanywa kuwa kama kichaka cha kuhifadhia magari mabovu
‘’Magari
haya hayaridhishi katika ubora wake sasa lengo letu sisi ni kuhakikisha kuwa
kila chombo kinapokuwa barabarani kiwe kimekidhi vigezo sasa haya magari ya
shule, mengi yamefanywa ni kichaka cha kuhifadhia magari mabovu, yaani mmiliki
akishindwa ushindani wa kazi za daladala kutokana na hali ya gari yake imekuwa
siyo nzuri sana anaikimbiza kwenda kubebea wanafunzi ,huku wakiamini kuwa
hatuyakaguliwi mara kwa mara kwa kutokuharibu ratiba ya wanafunzi‘’Amesema
Mwangamilo
Mwangamilo
amesema awali waliwaandikia wamiliki wa shule hizo na kuwataka kupeleka idadi ya magari ,ila hadi ukaguzi unaanza bado
siyo wamiliki wote wamekuwa waaminifu kutimiza agizo hilo,bali inaonekana upo
ujanja unaotendeka kwa kuchagua magari yenye hali nzuri na kuyapeleka,baliJeshi la polisi limesema wao
wametimiza jukumu la kuyakagua magari hayo.
‘’Shule zina
magari mengi bado hayajafikia kiwango ambacho kipo katika magari ya shule ,ninachokiona
hapa kuna ujanja ujanja unatendeka kwa kuchagua magari yenye hali nzuri ndiyo
wameyaleta,sisi tunayakagua kutokana na viwango vyetu,ila niwaambie wamiliki wa
shule kuna magari ambayo wameyaficha hawataki kuyaleta kwaajili ya uchaguzi] na
wapate ushauri wa kiufundi’’
Aidha
amesisisitiza kuwa ukaguzi huo ni wa lazima kutoka ndani ya jeshi la polisi,hivyo
endapo watashindwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na jeshi hilo, magari hayo kuanzia
siku ya jumatatu 13 juni 2022,wataanza oparesheni katika kila eneo kuhakikisha kwamba yale magari ambayo hayana
hati ya ukaguzi yanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria
‘’Hatua hizi
zinaweza kwenda mbali sana hata mmiliki wa gari hilo anaweza kuchukuliwa hatua ,na gari yeyote ambayo itakutwa haina ripoti
ya ukaguzi itapelekea sisi kutambua kuwa lilikuwa gari limefichwa wakati
yalipohitajika kwa ukaguzi.
Aidha
ukaguzi huo wa siku mbili wa magari ya kubeba wanafunzi (school bus)umeanza leo
jumamosi utamalizika siku ya kesho jumapili 12juni 2022 ili kutokuvuruga
utaratibu wa wanafunzi,unaendelea katika halmashauri ya Jiji la Arusha,arusha
Dc,Arumeru na Longido .