Na Zulfa Mfinanga,
Moshi.
Jukwaa la Sera limekutana leo mjini Moshi kwa lengo la kuangalia sera na sheria zinazokwamisha vita dhidi ya ukatili wa kingono kwa Wanawake na watoto.
Jukwaa hilo litakaa kwa muda wa siku mbili likiwashirikisha wanaharakati wa Haki za Binadamu kutoka Wilaya ya Moshi na Siha za Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na wanaharakati kutoka Wilaya ya Arusha na Meru Mkoani Arusha.
Akielezea maana ya Jukwaa la Sera, Mkurugenzi wa Shirika la Deploy & Nurturing Gallery (DNG-Tanzania) Nhojo Kushoka amesema ni shughuli ya utoaji Elimu ya Haki za Binadamu ambayo inatoa fursa kwa jamii, wawakilishi wa mashirika ya wanawake na mashirika ya Haki za Binadamu kujadili sheria na/au sera ambazo zinashughulikia ukatili wa kingono kwa wanawake na watoto.
“Lengo la Jukwaa la Sera ni kuandaa mpango Kazi wenye kuboresha utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili kwa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) katika kushughulikia changamoto na mapungufu ya mpango huu kwa kushirikisha mashirika, watoa maamuzi pamoja na jamii husika”
Mkurugenzi wa Shirika la Women Empowerment and Gender Support (WEGS) Joyce Mwanga, akiwaelezea washiriki hao juu ya Mradi wa Kukuza Usawa kwa kutumia Elimu ya Haki za Binadamu ambapo alisema kuwa katika nchi ya Tanzania jitihada nyingi zimefanyika kulinda haki za msingi za binadamu lakini bado hakuna usawa hasa kwa wanawake na wasichana.
Bi. Mwanga amesema lengo la mradi huu ni kuona ongezeko la uwezo wa wanawake na watoto wa kike katika Kukuza Usawa wa kijinsia ndani ya jamii.
Wakichangia changamoto zinazotokana na Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili kwa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) mwezeshaji wa Jukwaa hilo Evarester Mlamie amesema jamii husika ambayo ndiyo waathirika wa vitendo vya ukatili wa kingono haikuhisishwa kwenye kamati za MTAKUWWA ngazi ya Kata.
|
Washiriki wa Jukwaa la Sera ambao ni wanajamii, viongozi wa dini, viongozi wa mila, watumishi wa Umma pamoja na mashirika ya Haki za Binadamu wakiendelea na majadiliano juu ya mada mbalimbali za kutokomeza ukatili wa kingono kwa Wanawake na watoto. |
|
washiriki wakifuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea |
|
washiriki wakifuatilia mjadala |
|
Wageni kutoka shirika la Equitas la nchini Canada pamoja na Shirika la Women Empowerment Link la nchini Kenya nawakisikiliza mada zilizokuwa zinatolewa kwenye Jukwaa la Sera |
|
wageni wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa |
|
Mkurugenzi wa Shirika la Deploy & Nurturing Gallery (DNG-Tanzania) Nhojo Kushoka akielezea washiriki nini maana ya Jukwaa la Sera pamoja na malengo ya Jukwaa hilo. |
|
Mkurugenzi wa Shirika la Women Empowerment and Gender Support (WEGS) Joyce Mwanga, akiwaelezea washiriki juu ya Mradi wa Kukuza Usawa kwa kutumia Elimu ya Haki za Binadamu |
|
Mkurugenzi wa shirika la Community Economic Development and Social Transformationn (CEDESOTA) Jackson Muro akiwasilisha mada katika mkutano huo |
|
Washiriki kutoka kata ya maruvango wilaya ya Meru Mkoani Arusha |
|
Washiriki kutoka kata ya Biriri Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro |
|
Washiriki kutoka kata ya Sokoni 1 katika Wilaya ya Arusha Mkoani Arusha |
|
Washiriki kutoka kata ya Bomambuzi Wilaya ya Moshi Kilimanjaro
|